February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

OLENGURUMWA ATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WILLIAM TATE OLE NASHA

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),Onesmo Olengurumwa hii leo ametia saini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro,William Tate Ole Nasha.Msiba huo upo nyumbani kwa Marehemu eneo la Medel NHIC Dodoma.

Olengurumwa akiwa ni miongoni mwa wenyeji wa Ngorongoro ameeleza kuwa Olenasha enzi za uhai wake alifanya mambo mbalimbali katika jimbo hilo hususani miradi ya maendeleo katika sekta ya maji,elimu na maeneo mengine mengi.

Aidha Olengurumwa ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu,jamaa wa Marehemu na wananchi wa Ngorongoro kwa kumpoteza mbunge wao.

William Olenasha alizaliwa mnamo mwaka 1972 katika kijiji cha Kakaesio Wilayani Ngorongoro na amefariki dunia hapo jana tarehe 27/09/2021 nyumbani kwake jijini Dodoma.