Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kimelaani vikali matukio ya mauaji yanayoendelea hapa nchini na kuitaka jamii kutojihusisha nayo.
Katika tamko lililotolewa na OJADACT hii leo Mei 31,2022 na kutiliwa saini na Mwenyekiti wake,Edwin Soko imetoa wito kaa serikali Kufanya tafiti za kina kubaini vyanzo vya mauaji hayo pamoja na kuanzisha vituo vya kisaikolojia.
“Wanandoa watarajiwa wawe na muda wa kujuana tabia kwa undani kabla ya kuoana na kufuata mifumo rasmi ya usuluhishi wa matatizo yao,”imesema taarifa hiyo.
Aidha OJADACT imelitaka Jeshi la Polisi nchini kutoa elimu sahihi ya matumizi ya silaha kwa wamiliki wa silaha nchini pamoja na kuwataka wazazi kuhakikisha wanajihusisha na malezi ya watoto wao na kuepuka kuwaacha watoto hao wajilee kimaadili.
Taarifa hiyo ya OJADACT imesema matukio hayo ya mauaji yamesababisha baadhi ya watu kutolewa na kukatishwa uhai wao kinyume na Ibara ya 14 Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayotoa haki ya mtu kuishi.
“Matukio hayo (ya mauaji) yamegawanyika katika makundi mbalimbali , yapo mauaji yaliyofanyika kwa sababu za kimapenzi, tuhuma za wizi na imani za kishirikina,”imeeleza .
-Endelea kufuatilia @watetezitv Kwa habari kemkem za kuhabarisha,kuelimisha na masuala ya haki za binadamu saa 24
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA