February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

OFISA WA POLISI AJICHIMBIA KABURI

Katika hali ya kushangaza Ofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Patrick Matey Kimaro (59)  amejijengea  kaburi lake mwenyewe lililogharimu kiasi cha shilling Milioni 4, ili kuepusha usumbufu kwa familia yake pale atakapofariki.Kaburi hilo amelijenga nyumbani kwake wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na kusema

“hili ni kaburi langu nimelitayarisha na kulichimba mwenyewe kwa hiyari yangu sikulazimishwa na mtu yeyote nimelijenga nikiwa na akili timamu

Kimaro ameeleza kwa namna kazi yake ilivyo amekutana na mambo mengi ambayo yamemfanya afikia uamuzi huo kwakuwa kifo kipo na pia kwa kuangalia maandiko yanavyosema.

“Lakini pia nimefikiria mambo mengi kwamba hii dunia ni ya kupita na naangalia maandiko yanasemaje mm ni mkristo umri wa mwanadamu anayezaliwa umri wake wa kuishi ni miaka 70 ikizidi ni 80 sasa nna miaka 59 nakarinbia 60 na pengine mwaka kesho kama Mungu akipenda nitafikia mwisho wangu wa utumishi” amesema