Aliyewahi Kugombea Urais kwa Tuiketi ya Chadema mwaka 2010,Dkt Wilbroad Slaa amesema alipitishwa kugombea nafasi hiyo kwa bahati mbaya baada ya mipango ya kumpata Samuel Sitta kama mgombea wao kugonga mwamba.
Dkt Slaa amezungumza hayo akiwa katika mahojiano maalum na Dar 24 media na kueleza kuwa akiwa kama Katibu Mkuu CHADEMA na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alipewa jukumu la Kutafuta Mgombea atakayesimama kupeperusha bendera ya CHADEMA.
“Nilifanya kazi hiyo kwa uaminifu na uadilifu mkubwa bila kujiwekea mimi binafsi nafasi ya kwenda kugombea bahati mbaya mipango hiyo ilikuja kufeli dakika ya mwisho”amesema Dkt Slaa
Aidha ameongeza kuwa baada ya kumkosa Samuel Sitta alipitishwa na Kamati Kuu kugombea nafasi hiyo dakika za mwish.
“baada ya mipango hiyo kushindikana mimi nikaombwa dakika ya mwisho ndani ya Kamati Kuu nikathibitishwa kwamba mgombea wetu atakuwa Dkt Slaa na nilitoka katika kikao kile nikaenda kulala kwa siku mbili ninaumwa” ameongeza
Habari Zaidi
UFAFANUZI WA KISHERIA KUHUSU ARDHI YA LOLIONDO
WANAOJISAIDIA VICHAKANI HATARINI KUPATA MAGONJWA YA TUMBO
MONGELA AIBUA TENA SAKATA LA MGOGORO WA ARDHI LOLIONDO