February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

NI HUKUMU YA KIHISTORIA ALIYEMUUA MMAREKANI MWEUSI ,GEORGE FLOYD

Derek Chauvin-Askari aliyemuua George Floyd

Na Leonard Mapuli.

Mahakama ya Mjini Minneapolis,Minnesota nchini Marekani imemhukumu afisa wa polisi Derek Chauvin miaka 22.5 jela baada ya kumkuta na hatia katika mauaji ya Mmarekani Mweusi yaliyotikisa dunia kwa maandamano kuanzia mwezi May,mwaka 2020.

Anakwenda jela baada ya Mahakama ya Minnesota kujiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa Derek alitenda makosa ya Kutumia vibaya nafasi aliyoaminiwa nayo pamoja Mamlaka yake,Ukatili dhidi ya Floyd,Kutenda kosa hadharani huku watoto wakishuhudia,na kutenda kosa kwa kushirikiana na watu wengine (Watatu),ambapo yote haya kinyume na sheria za Minnesota.

“Ninatoa salamu zangu za pole kwa familia ya Floyd”,haya yalikuwa maneno ya mwisho ya Derek kabla hukumu yake kusomwa.

Kwa mujibu wa sheria za Minnesota, Derek atatakiwa kutumikia robo tatu  au miaka 15 ya kifungo jela.

Kwa nini ni hukumu ya kihistoria

Kwa mujibu wa muongozo wa utoaji adhabu mjini Minnesota,mtu anapaswa kufungwa jela kwa muda usiozidi miaka kumi hadi 15 ,ikiwa ni kiwango cha juu mno cha  adhabu dhidi ya makosa ya jinai,lakini kwa Derek muongozo huo umewekwa kando na Deriki atatumika adhabu kwa miaka 22 na miezi 6..

Jaji aliyesikiliza kesi hiyo Peter Cahill amesema adhabu hiyo haijafuata mihemko wala mawazo ya  watu.

“Nimezingatia zaidi maumivu ambayo familia ya Floyd imeyapata na inayo hadi leo” ameandika Jaji Cahill katika hukumu hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa 22,ikitajwa kuwa hukumu kali mno  kwa Derek ,anaedawili pamoja na mkosa mengine, kutumia vibaya nafasi yake pamoja na mamlaka aliyopewa.Katika hukumu hiyo,Jaji Cahill amesema Derek bila heshima alimdhulumu Floyd “Utu” waake ambao ni haki ya kila binadamu.

Picha ya video iliyomuonesha Derek akimkandamiza shingo Floyd bila kumpa nafasi hata ya kupumua kwa muda mrefu,ni dhahiri alimsababishia maumivu yasimithilika,”Yalikuwa mauji ya maumivu na mateso ya kiwango cha Juu sana”, inasomeka sehemu ya hukumu ya Jaji Cahill.

Watu wakifurahia hukumu ya aliyemuua Floyd

Kesi hii pia inabaki kuwa historia katika mwenendo wa usikilizwaji wake ambapo baada ya kumkuta Derek na hatia, jopo la waendesha mashtaka wa serikali lilipendekeza apewe adhabu ya miaka 30 jela hatua ambao jopo hilo lilisema inaweza kuifuta zaidi mochozi familia ya Floyd na jamii ya watu weusi.

Derek ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kutazama historia yake kuwa hana historia yeyote ya kutenda makosa nchini humo,huku wenzake watatu walio nae eneo la tukio Tou Thao,Thomas Lane,na Alex Kueng wakitarajiwa kupandishwa kizimbani mwezi March mwaka 2022.

Akiwa na wenzake Derek alimuua George Floyd kwa kumbana shingo kwa nguvu akitumia goti kwa muda wa dakika 9 na sekunde 29 bila kumpa pumzi  na alisikia  kilalama kwa mbali kuwa hawezi kupumua alipokamatwa na askari huyo kwa madai ya kufanya malipo katika duka moja kwa kutumia noti bandia.

Vitendo vya polisi kuua raia ncni marekani Marekani vimekuwa vikiongezeka siku mara kwa mara,ndani ya miezi mitano ya mwaka 2021,watu 371 wamefyatuliwa risasi na polisi,kati yao 71 wakiwa  watu weusi.Mwaka 2020  hali inatajwa kuwa mbaya zaidi ambapo watu 1,021 walipigwa risasi na polisi.Katika matukio hayo  ndani ya miaka miwili,idadi ya wamarekani weusi inaongoza kwa kushambuliwa kwa risasi na polisi ikiringanisha na makundi mengine yanayopatikana nchini humo.