February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

NGO MKAKATI MPYA WA MIAKA MITANO 2022/2026

Na: Anthony Rwekaza

Baada ya mpango mkakati wa awali wa miaka mitano kutoka 2016/2020 kukamilika licha kuongezewa mwaka mmoja mpaka Desemba 2021, Shirika lisilo la Kiserikali la Legal Services Facility (LSF) hapo jana , 21, Augosti 2021 limezindua mpango mkakati wa mpya wamiaka mingine mitano 2022/2026.

Akizungumza wakati wa uzinduzi mpango mkakati Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakila amesema mpango wa miaka mitano waliozindua unalenga kutoa mwelekeo endelevu wa shughuli za shirika hilo Nchini Tanzania kwa kuwezesha wananchi haki zao.

” leo tunayofuraha kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano ambao umelenga kutoa mwelekeo endelevu ya shughuli zetu Nchini za kuwawezesha wananchi kupata haki zao” amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakila

Pia Ng’waikila amesema kuwa mpango huo umejikita katika kuchangia mpango wa maendeleo endelevu ya Dunia (SDG) SDG 16 unaolenga kuleta haki na kuboresha usawa wa kijinsia na kuwainua Wanawake na wasichana

“Mpango huu umejikita katika kuchangia mpango mpango wa maendeleo endelevu ya Dunia (SDG), SDG 16 uliolenga kuleta haki kwa wote na SDG 5 inayolenga kuboresha usawa wa kijinsia na kuwainua wanawake na wasichana, sambamba na malengo na malengo endelevu ya Dunia pia uchangia katika mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya Taifa 2016/2017 -2020/2021.

Ng’wanakilala pia alianisha maeneo makuu yatakayopewa kipaombele ambayo ni, kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za musaada wa kisheria, hususani kwa wanawake, kujenga uelewa kwa jamii juu ya Sheria na haki zao hususani Wanawake, kuboresha mazingara ya endelevu ya upatikanaji wa haki, kuimarisha taasisi na sekta ya msaada wa kisheria kuwa endelevu.

Aidha kwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mpango huo, Msajili wa taasisi zisizo za kiserikali (NGO) Tanzania Bara, Vickness Mayao, wakati akitoa hotuba ya uzinduzi amesema amefurahishwa kuona LSF imekuja mpango mkakati mpya wa miaka mitano.

Ameongezea kuwa inainyesha wazi kuwa ‘program’ ya upatikanaji wa haki itaendelea kutekelezwa suala litainufaisha Serikali chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, na amelipongeza Shirika hilo kwa kushirikiana vyema na ofisi yake na kuweka wazi mchango wa LPF kwenye mashirika mengine ambayo yamesajiliwa.

” LSF ni mdau wetu mkubwa na moja kati ya NGO zinazofanya kazi kwa karibu kwa kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto zinazopelekea wananchi hususani wanawake kupoteza haki zao na wamekuwa wakitoa ruzuku kwa mashirika ambayo mengi amabayo tumeshayasajili sasa kwa mujibu wa sheria, hivyo nawapongeza sana kwa hatua nyingi tunayoipiga leo” amesema Msajili wa NGO Tanzania bara, Vickness Mayao.

Aidha Vickness ameeleza kuwa LSF imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa Serikali katika mpango wa kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto (NPA-VAWC) kwa wadau wake kutoa msaada wa kisheria, pia ushirikiano huo unaendelea kwenye mchakato wa kufanyia marekebisho sera ya Wanawake ya mwaka 2000 ambayo pindi ikikamilika itasaidia kulinda zaidi maslahi ya wanawake, pia ametoa rai kwa wadau mabalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kama wanavyofanya LSF.

Katika mpango mkakati ulioanzwa kutekelezwa mwaka 2016-2020 umekuwa ukifadhiliwa na wadau wa maendeleo ikiwemo DANIDA, DFID, na EU, katika mpango mpya utakao anza kutekelezwa ni kuongeza wadau wengi zaidi ili kuweza kufikia maeneo mengi zaidi katika ngazi za Kata na Vijiji ambayo havijafikiwa na huduma za msaada wa kisheria bure bila gharama yoyote.