March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

NGO KUPELEKA MASHAURI MAHAKAMA YA AFRIKA, MSIMAMO KUANGALIWA UPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Rais Siylvain Ore na kuipongeza mahakama hiyo iliyopo Arusha Tanzania, kwa kazi inazozifanya.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Mei 27, 2021 Rais Samia amemuhakikishia Rais Ore kuwa serikali ya Awamu ya sita itampatia ushirikiano ikiwemo kushughulika na changamoto mbali mbali kwa kutambua umuhimu wa majukumu yake kwa wananchi wa Tanzania.

Pamoja na Ahadi za ushirikiano Rias Samia amempongeza Rais Ore kwa utumishi wake uliotumika kwa vipindi viwili katika mahakama hiyo na kumuomba kuwa balozi mwema wa Tanzania.

Rais Samia ameahidi kuangalia upya msimamo wa serikali uliofuta tamko la kuruhusu taasisi zisizo za kiserikali (NGO) kupeleka mashauri yao moja kwa moja katika mahakama hiyo japo mpaka sasa msimamo haujabadilika.