Ndege kubwa ambayo inamilikiwa na shirika la ndege la Eastern Airlines la China inayodaiwa kuwa ilikuwa imebeba watu 132,jimboni Guangxi imeanguka, ambapo maafisa wa China wamethibitisha tukio hilo.
Kwa mujibu taarifa kutoka katika Shirika la Anga la China (CAA), Ndege ni kuwa Ndege hiyo ilikuwa na abiria 123 na watumishi 9.
Hata hivyo mpaka taarifa hii inaripotiwa kwenye vyanzo mbalimbali bado taarifa rasmi za chanzo cha ajali hiyo na kiwango cha athari havijajulikana
Imeripotiwa na Shirika la habari la China ambapo limedai kuwa ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ilipata ajali kwenye mji wenye milima wa Wuzhou, lakini mlipuko wa moto umeshuhudiwa kwenye mapori yanayozunguka eneo hilo ambapo inadaiwa kuangukia.
Jitiahada za uokozi zimeanza ikiwa tayari China imeshatuma vikosi vya uokoaji l kwenda kutoa msaada kwenye eneo hilo.
Inaelezwa na baadhi ya vyanzo vya taarifa kuwa Ndege hiyo yenye usajili wa MU5735 iliondoka kwenye mji wa Kunming majira ya saa 7:11 mchana ikiwa ni kwa saa China na ambapo ilitarajiwa kuwasili saa 9:05.kwenye mji wa Guangzhou .
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS