February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

NAPE ASEMA GHARAMA ZA DATA ZIMEPUGUA TOKEA RAIS SAMIA AINGIE MADARAKANI

Kufuatia mjadala wa kupanda kwa gharama za vifurushi kwa watumiaji wa data kwenye mitandao ya kijamii Waziri ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kupitia Ukurasa wake wa Twitter ametoa ufafanuzi kwamba Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuingia madarakani alichukua hatua ya kushusha gharama za data, ambapo amedai kuwa awali Machi 2021 bei ya juu ilikuwa ni Tsh. 40.04 lakini amesema kuwa ilipungzwa na kufikia Agosti 2022 bei ya juu ni Tsh. 9. 35
Kumekuwepo na mjadala kupitia mitandao ya kijamii hususani Twitter, Jamiiforums na kwenye kurasa nyingine kuhusu kupanda kiolela kwa gharama za vifurushi vya mitandao ya simu ikiwemo gharama za data.
Baadhi ya wadau wakiwemo wanaharakati wamekuwa wakieleza maswali na hoja zao hasa kwa Waziri Nape ambaye anayodhamana ya kusimamia wadau hao ambao utoa huduma za mawasiliano, Kati ya wadau hao wapo baadhi ambao hawalizishwi na namna suala hilo linavyochukuliwa.
Itakumbukwa watumiaji wa Internet Nchini Tanzania wamekuwa wakiongezeka ambapo kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) walitoa ripoti ya takwimu mpya za robo ya nne ya mwaka 2021, takwimu hizo zinaonesha kuwa Watumiaji wa intaneti wanazidi kuongezeka Tanzania kufikia milioni 29.8 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 ambalo ni sawa asilimia 4.4 kutoka milioni 28.5 kwa mujibu wa takwimu za robo ya mwisho ya mwaka 2020.