March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MWILI WA MUGABE KUZIKWA UPYA

Hayati Robert Mugabe enzi za Uhai wake.

Kiongozi mmoja wa kimila nchini Zimbabwe ameamuru mabaki ya mwili wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe yafukuliwe na kuzikwa upya katika makaburi ya mashujaa mjini Harare na kwamba uamuzi wa alipozikwa sasa ulichangiwa kwa kiasi na mke wake.

Mugabe aliyeondolewa madarakani kwa Mapinduzi ya mwaka 2017 kabla ya kifo chake mwaka 2019 alizikwa katika kijiji chake cha Kutama baada ya mvutano uliodumu kwa majuma kadhaa kati ya serikali ya rais Emmerson Mnangagwa na familia ya Mugabe.

Viongozi wa kimila (Machifu)wanaruhusuhiwa kwa mujibu wa sheria kufanya maamuzi kama hayo katika maeneo wanakotawala ila imekuwa mara chache sana kushuhudia uamuzi kama huu wa kufukuwa na kuzika upya mwili uliokweishazikwa kitambo.