February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MWENENDO KESI YA MBOWE NA WENZAKE, SHAHIDI UTETEZI ADAI HAWAJUI HALIPO MWENZAO MOSES LIJENJE, USHAHIDI KESI NDOGO WAKAMILIKA, UAMUZI KUTOLEWA OKTOBA 4, 2021

Na: Anthony Rwekaza

Kesi Na.16/2021 yenye mashtaka ya Ugaidi, inayomkabili Freeman Mbowe pamoja na wenzake, Halfan Hassan Mbwire, Adam Hassan Kasekwa(anadaiwa alikuwa komandoo wa JWTZ), Mohamed Ling’wenya (anadaiwa pia alikuwa Komandoo wa JWTZ), imekuwa ikisikilizwa kwa mfululizo kwenye Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na makosa ya Rushwa kabla ya Jumatano Septemba 29, 2021 kuahirishwa mpaka Oktoba 19, 2021.

Mnamo Oktoba 19, 2021 kwenye Mahakama hiyo mbele ya Jaji Mstapha Siyani anayesikiliza Kesi hiyo anatarajiwa kutoa uamuzi wa Kesi Ndogo kwenye ya Msingi, uamuzi huo unakuja ikiwa ni baada ya Upande wa utetezi kupitia jopo la mawakili wakiongozwa na Wakili Peter Kibata kupinga kupokelewa kwa kielelezo cha maelezo ya mshtakiwa wa Adam Kasekwa kutochukuliwa na Mahakama kwa kwa madai kuwa maelezo ya mshtakiwa kwa madai kuwa maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda kisheria aliteswa kabla na wakati akichukuliwa maelezo.

Kesi hiyo ndogo imeibua sura tofauti ambapo mashaidi watatu wa upande walitoa ushaidi wao akiwemo Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Ramadhani Kingai ambaye anadiwa kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa msafara wa kuwatoa watuhumiwa Moshi na kuongoza mchakato wa kuchukua maelezo, Inspecta Omari Mahita, Constable Msemwa, awali Jamhuri ilipanga kutumia mashahidi saba kabla ya kuiambia Mahakama kuwa inatoa ombi la kufunga ushahidi wake baada ya mashahidi wake watatu kumaliza kutoa ushahidi.

Baada ya wa Jamhuri kuitimisha kutoa ushaidi wake, upande wa utetezi nao umekamirisha kutoa ushahidi wao kupitia mashaidi watatu wakiongozwa na mshtakiwa Adam Kasekwa ambaye ni ndiye msingi wa kesi hiyo ndogo, mshtakiwa Mohamed Ling’wenya na Mke wa Adam, Liliani Kibona. Mawakili wa pande zote mbili Utetezi na Jamhuri wamekubaliana kuwasilisha majumuhishi ya hoja kwa njia ya maandishi siku ya Jumatatu Ocktoba 4, 2021.

Kesi hiyo Ndogo imekuwa ikuvuta hisia za watu mbalimbali wakiwemo maafisa wa Balozi wanaoziwakirisha Nchi zao Nchini Tanzania, viongozi wa Chadema na viongozi wa vyama vya siasa Nchini Tanzania, Wanaharakati, Wanahabari pamoja na Wananchi kufika kwenye viunga vya Mahakama hiyo iliyopo eneo Mawasiliano Jiji Dar es salaam kwenye chuo cha Sheria, ambapo ulinzi umekuwa ukiimarishwa kila washtakiwa hao wanapoletwa Mahakamani.

Ikumbukwe Kesi hiyo awali ilianza kusikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam ambapo washtakiwa hao walisomewa mashtka sita ikiwemo kula njama za kutenda ugaidi, ikiwemo kupanga kulipua vituo vya mafuta, kukata miti na kuiweka barabarani, kudhuru viongozi, kwa madai kuwa lengo Nchi hisitawalike kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2020, ilielezwa hivyo wakati watuhumiwa wakisomewa mashtaka mbele ya Mahakama.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo kwa taratibu za kisheria, Hakimu Thomas Simba aliamishia kesi hiyo kwenye Mahakama ya Kuu, ambapo makosa hayo yaliwekwa kwenye Divisheni ya Uhujumu Uchumi, na ilianza kusikilizwa kwenye Mahakama hiyo na Jaji Elineza Luvanda ambaye alikuja kuridhia ombi la kutaka hajitoe lililowasilishwa na upande wa utetezi kwa madai kuwa hawana imani naye kwenye kusimamia kesi hiyo.

Hatua hiyo ilikuja mara baada ya Jaji Luvanda kutupilia mbali pingamizi zilizowekwa na mawakili wa utetezi dhidi ya Jamhuri kwenye shauri hilo, hali hiyo ilipelekea kesi hiyo kuahirishwa ili kuruhusu mchakato wa Mahakama kumteua Jaji mwingine na kupanga siku ya kesi kusikilizwa tena. Baada ya mchakato huo kukamilika ilitolewa taarifa kuwa Jaji Mstapha Siyani kupewa jukumu la kusikia Kesi hiyo na kuweka wazi siku ya kesi kuanza kusikilizwa tena.

Katika sehemu ya maelezo ya upande wa utetezi shahidi wa pili Mohamed Ling’wenya alidai mtu mwingine ambaye alimtamburisha kwa jina la Moses Lijenje waliyekuwa naye kwenye maeneo waliyokamatiwa hajulikani alipo mpaka wakati huo alipokuwa akitoa ushahidi wake na bado hajajumuishwa kwenye kesi hiyo, lakini kwa maelezo katika ushahidi uliotolewa na Kamanda Kingai ni kuwa mtu huyo alikimbia kwenye harakati za kutaka kumkamata. (Hali hiyo imeanza kuibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikihoji, wapi alipo Moses Lijenje)

Washtakiwa watatu kwenye kesi hiyo inadaiwa walikamatwa Agosti 5, 2021 Mkoani Moshi na kusafirishwa mpaka Dar es salaam, huku wakikaa gerezani kwa zaidi ya miezi nane, ikiwa upande wa mashtaka ulidai kuedelea na upelelezi wa tuhuma zilizowakabili watuhumiwa hao, huku Freeman Mbowe alikamatwa June 21, 2021 akiwa Mwanza na kusafirishwa mpaka Dar es salaam kabla ya kupelekewa Mahakamani na kujumuhishwa kwenye tuhuma zilizokuwa zikiwakabili washtakiwa hao wengine.

Upande wa Jamhuri umekuwa ukiongozwa na jopo la mawakili wakiwemo, Robert Kidando, Nassoro Katuga Ignas Mwanuka, Esther Martin, Tulimanywa Majigo​, huku upande wa utetezi umekuwa ukiwakilishwa na jopo la Mawakili, Peter Kibatala, Jonathan Mndeme, Fredrick Kiwhelo, John Malya, Sisty Aloyce, Alex Masaba, Idd Msawanga, Gaston Garubindi, Evaresta Kisanga, Faraj Mangula​, Maria Mushi, Bonifasia Mapunda​.