March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MWANZA: WATU 9 MBARONI TUHUMA ZA MAUAJI.

SACP. Ramadhan Ng'anzi-Kamanda wa Polisi (M)-Mwanza.

Respicius Kaiza.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu wanne ambao:- Robert Daud, miaka 42, mume wa mganga, mkazi wa katunguru, Sylivester Renetus, Miaka 30, Mkazi wa katunguru, Ryabakamba Sekelwa, Miaka 30, mwanamke, mganga wa kienyeji, mkazi wa katunguru na Elizabeth Jackson, miaka 23, wote wakazi wa Katunguru Senegerema,  kwa tuhuma za Mauaji ya Respikius Anastaz, Miaka 55, Dereva taxi aliyekua anapaki maeneo ya Dampo-mwanza, Mkazi wa Isamilo Mwanza, aliyeuawa ndani ya gari aina ya IST rangi nyeusi yenye namba T.143 DHV, kwa kukabwa na kamba, kuchomwa visu shingoni na kutobolewa macho hadi kufa, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

“Tukio hilo limetokea 26.01.2022 majira ya nne usiku katika kijiji cha Kasungamile, Wilayani Sengerema, hii ni baada ya Dereva tax ambaye ni Marehemu kwa sasa kukodiwa na mtuhumiwa Sylivester Renatus akiwa na mkewe Elizabeth Jackson toka Buzuruga Mwanza kwenda Sengerema na walipofika maeneo ya Kijiji cha Kasungamile walitekeleza unyama huo. Inadiwa kuwa baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kwa mganga wa kienyeji ili wasafishwe aitwaye Ryabakamba Sekelwa ambaye amekamatwa pamoja na mumewe” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Ramadhan Ng’anzi amewambia wandishi wa Habari.

Gari la Marehemu Respikius lilivyoktwa na namba feki,baada ya Marehemu kuuawa,wilayani Sengerema.

Polisi wakiwa doria majira ya saa nne usiku, walikuta gari hiyo ikiwe imetelekezwa katikati ya barabara ndipo ufuatiliaji wa haraka ulifanyika na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa pamoja na mganga wa kienyeji. Kiini cha tukio hilo ni kuwania mali (kupora gari). Tayari gari imepatikana ikiwa imefungwa namba bandia  mbele na nyuma ambayo ni T 620 CGN na  eno la tukio kumepatikana Visu viwili, panga moja, nyundo moja na simu mbili aina ya TECNO moja kubwa na nyingine ndogo na kamba moja.

Katika tukio jingine, kijana Nicholus Telesphory (25), Mkazi wa Malimbe na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt.Augustine –Mwanza, aliuawa na kundi la wahalifu kwa kupigwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali  za mwili wake  kwa tuhuma za wizi wa Televisheni na baadae kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika  hospital ya Mkoa Sekou Toure.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Ramadhani Ng’anzi akionesha baadhi ya silaha zilizotuika katika mauaji.

Tukio hilo limetokea mnamo Januari 29 mwaka 2022 majira ya saa moja na nusu usiku, huko mtaa wa Ng’washi, kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana,

Baada ya upelelezi wa kina Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa  watano kuhusiana na tukio hilo ambao ni Thobias Lucus Joseph, miaka 25, mkazi wa Nyanembe, Alex Madoshi Junior, miaka 20, Mkazi wa Ng’washi, Yusuph Mwandesha, miaka 25, mkazi wa Ng’washi, Samwel Masalu George, Miaka 25, mkazi WA Lwanhima na Nyanda Madirisha, miaka 19, Mkazi wa

Ng’washi, wote ni waendesha bajaji.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linakamisha upelelezi wa mashauri haya na baadae watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao” Amefafanua SACP Ramadhan Ng’anzi.

Aidha,jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa onyo kwa baadhi ya wananchi wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuwania mali kuacha mara moja kwani ni kosa kisheria na endapo watabainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Sambamba na hilo linawasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kudhibiti vitendo vya kihalifu na wahalifu katika Mkoa wetu.