March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MWANDISHI MABALA: KITABU KIPYA KITAKUWA NA MAMBO HAYA

Na Antony Benedicto

Mwandishi mkongwe wa vitabu, Richard Mabala ameelezea maudhui yaliyoko kwenye kitabu cha HakiElimu kinachotegemewa kutolewa kwa umma hivi karibuni.

Amesema Kitabu hicho kimeelezea historia pana ya mabadiliko ya sekta ya elimu Nchini Tanzania tokea kipindi cha ukoloni mpaka walipofikia uamuzi wa kuanzisha taasisi ya HakiElimu mpaka wakati ambao taasisi hiyo inapoadhimisha miaka 20 tokea ilipoanzishwa.

Aidha mwandishi huyo ambaye anasifika kwa kuchapisha vitabu tofauti ambavyo vinatumika kwenye mitaala ya elimu Nchini Tanzania, amesema HakiElimu imeleta mageuzi makubwa kwenye elimu kutokana na kushirikiana vyema na wadau ikiwemo Serikali.