March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO

Mahakama nchini Rwanda imetupilia mbali shitaka la ubakaji linalomkabili ya muandaaji wa shindano la Miss Rwanda, Dieudonné Ishimwe kna kusema atafunguliwa mashtaka mengine ya uhalifu wa kingono.
Ishimwe alikamatwa mwezi uliopita na kushitakiwa kwa ubakaji na kuomba ngono ili kutoa upendeleo kwa washiriki wa mashindano hayo,Hakimu alisema hakuna ushahidi wa kutosha wa kumshitaki kwa ubakaji lakini atakabiliwa na mashitaka ya kuomba upendeleo wa kingono na unyanyasaji wa kijinsia.
Hata hivyo Ishimwe amekanusha mashitaka yote yanayomkabili.
Serikali ya Rwanda juma lilipoita lilisitisha mashindano hayo ya urembo baada ya mwandaaji wake kukamatwa.