February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MWALIMU ANAYETUHUMIWA KULAWITI WANAFUZI DAR APANDISHWA KIZIMBANI

HATIMAYE Mwalimu wa Shule ya Msingi Global International School, ya jijini Dar es Salaam, Daniel Magere, anayetuhumiwa kwa kulawiti na kubaka baadhi ya wanafunzi wake, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kujibu tuhuma zinazomkabili.
Mwalimu Magere amepandishwa kizimbani hapo leo Jumanne, ambapo amesomewa mashtaka sita na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hilda Kato, mbele ya Hakimu Mkazi, Frankoo Kiswaga. Hata hivyo, amekana mashtaka hayo.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Serikali kuingilia kati sakata hilo, kufuatia baadhi ya wazazi wa watoto hao kuibuka hadharani na kufichua tuhuma zinazomkabili Mwalimu Magere.
Akimsomea masbtaka hayo, Wakili Kato amedai mshtakiwa waliwatendea vitendo hivyo wanafunzi wa kike watatu wenye umri kati ya miaka mitano hadi saba, katika nyakati tofauti kuanzia Januari hadi Mei, 2022.
Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Mwalimu Magere, kuwanyanyasa kingono baadhi ya wanafunzi wakiwa shuleni kwa kuwalazimisha wamnyonye sehemu zake za siri kwa lengo la kujiridhisha kingono.