February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MUME AMUUA MZEE “MCHEPUKO” WA MKE WAKE

Na Leonard Mapuli.

Mwanaume mmoja (40) mkazi wa kijiji cha Teso,Kusini mwa kaunti ya Busia nchini Kenya anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Andungosi baada ya kumpiga na kumsababishia umauti mzee wa miaka 70 anaedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na moja ya wake zake.

Stephen,mwenye wake watatu,anadai marehemu  amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake mmoja kwa muda mrefu kabla ya kumfamania.

Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa,ni kwamba Marehemu alienda nyumbani kwa mke wake huyo na alipofika aliingia ndani na kupitiliza chumbani moja kwa moja bila kujua kuwa nae alikuwa ndani.

Kwa kinachoaminika kuwa ni mtego,Mtuhumiwa anasema siku hiyo alifika nyumbani mapema na aliegesha  piki piki yake katika nyumba jirani ili kumuaminisha marehemu endapo angekuja  kuwa hakuwepo mahali hapo.

 “Nilienda kulala majira ya saa nne usiku,ilipofika saa tano nilisikia mtu akinyata na kutembea ukutani kwenye nyumba yangu,baada kama ya robo saa hivi alisukuma mlango na kuingia ndani,cha kushangaza akapitiliza chumbani kama nyumbani kwa mke wangu,nilipomsikia niliruka kitandani na kuanza kumkabili”,amesema Stephen wakati akitoa maelezo Polisi.

“Nilimkamata na kumvuta wakati wakati nikitafuta pa kuwashia taa,alijaribu kufungua mlango  ili akimbie,wakati akijaribu kutoroka nilimpiga kichwani mara mbili,nikampiga tena kwenye miguu akaanguka chini ndipo akaanza kujieleza kwangu na uhusiano wake na mke wangu”,ameeleza mtuhumiwa huyo wa mauaji.

Mtuhumiwa huyo pia amedai tabia ya marehemu kwenda kulala na mkewe imekuwa ya mara kwa mara na ndio maana alipofika alifungua mlango bila uoga.