February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MUHIMBILI YAKANUSHA KUREKODI VIDEO YA PROF J AKIWA MAHUTUTI

Na: Anthony Rwekaza

Kufuatia kuenea kwa kipande cha video (clip) kwenye midandao ya kijamii ikionesha sura ya mtu ambaye alitambulika kuwa ni Prof. Jay akiwa kwenye chumba cha watu wenye uangalizi maalumu (ICU) katika hospitali ya Muhimbili, Hospitali hiyo imekanusha kuhusika shutuma za kuhusika kurekoti ‘clip’ hiyo.

Video hiyo ambayo ilianza kusambaa Jumatano March 10, 2021 kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo, Facebook, Instagram pamoja WhatsApp, imeibua mjadala ikiwemo hoja za kushutumu hospitali hiyo kuhusika, jambo ambalo ni kinyume na taratibu.

Katika taarifa iliyotolewa na kusaniwa na Afisa Mawasiliano kwa Umma kwenye hospitali hiyo, imeeleza kuwa video hiyo imeenezwa na Mtandao wa kijamii wa Mange Kimambi ikionesha Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay ambaye anaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo.

Kuna video iliyosambazwa kwenye mitandao wa kijamii wa Mange Kimambi ikimuonyesha Ndugu. Joseph Haule amabaye anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga)” taarifa imeeleza

Taarifa imeueleza umma kuwa video hiyo haijarekodiwa na kusambazwa na hospitali hiyo, ambapo wamedai kuwa wanahudumia wagonjwa 3,400 kwa siku ikiwemo wananchi wa kawaida viongozi wakuu wa Serikali, wanasiasa wengine huku wakiwa wanazingatia taaluma, maadili, utu na faragha.

Katika taarifa hiyo wamesema kuwa wanakemea vikali kitendo kilichofanywa cha kurekodi video ya mgonjwa ambaye anapigania uhai wake katika chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalumu (ICU) na kusambaza kinyume na taratibu za hospitali hiyo.

Taarifa imeendelea kuwa kitendo hicho ni kiwango cha juu cha kukosa utu na maadili, huku wakitoa pole kwa Prof. Jay pamoja na familia yake kufuatia kitendo hicho.

Wamewatoa hofu wananchi wanaotumia hospitali ya Mhimbili (Upanga na Mloganzila) kuwa waendelee kuwa na imani ya kutumia hospitali hiyo.

Wameongeza kuwa wanafuatilia kwa ukaribu kwa kuwasiliana na mamlaka husika ili kubaini chanzo cha video hiyo na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.

Itakumbukuwa Prof. Jay amekuwa hospilini hapo akipatiwa matibabu kwa zaidi ya Mwezi mmoja, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliweka wazi kugharamikia matibabu yake.