February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MTOTO WA MIAKA 16 MBARONI KWA TUHUMA ZA ULAWITI

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikilia kijana wa miaka 16( Jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumlawiti na kumsababishia kifo mtoto wa miaka minne.

Tukio hilo limeelezwa kutokea Novemba 10,2021 majira ya saa tatu asubuhi maeneo ya Chamazi Mbande katika Wilaya ya Temeke.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,Muliro Jumanne Muliro amesema uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo unaendelea na hatua za kisheria zitazingatiwa ili haki itendeke.