March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MTOTO WA MIAKA 14 ADAIWA KUWARAWITI WANZAKE 19 KWA KUWARUBUNI NA PIPI

Na: Anthony Rwekaza

Katika hali ya kushangaza Jeshi la Polisi mkoani Iringa limetoa taarifa kuwa linamshikilia mtoto mwenye umri wa miaka 14 kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wenzake 19 kwa wakati tofauti.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukimbi leo Machi 21, 2022, Amesema walifanya mahojiano na baadhi ya watoto wanaodaiwa kufanyiwa jambo hilo ambao nao walitaja wengine wakafikia idadi ya watoto 13, ambapo pia mtuhumiwa alikili kuhusika na madai hayo na kuwataja wengine sita na kufanya idadi kufikia watoto 19.

“Na hao watano walipohojiwa wakawataja wengine watano hivyo kufanya idadi ya watoto 13. Mtuhumiwa alipohojiwa alikubali na akawataja watoto wengine sita, wakawa 19,” amesema Kamanda wa Polisi, Bukumbi.

Pia amesema kuwa mtuhumiwa amekiri alikuwa akichukuwa fedha kwa bibi yake, na kununua pipi kama mbinu ya kuwapata wenzake ili awafanyie kitendo hicho ambacho ni kinyume na desturi pamoja na sheria, ambapo ameongeza mtuhumiwa huyo amekuwa akiwagawia pipi na biskuti wakati wakati watoto hao wakienda kungalia TV

“Kwa hiyo watoto walipokuwa wanaenda kuangalia TV aliwagawia pipi na biskuti kama njia ya kuwalaghai,” amesema Kamanda Bukumbi

Aidha amesema kuwa watoto wote waliotajwa walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa na Frelimo, ambapo amesema kuwa taarifa za kichunguzi ulibaini kuwa wamelawitiwa kama ilivyodaiwa.

Ameongeza kuwa Upelelezi wa sakata hilo umeshakamilika na atapelekwa Mahakamani kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria

“ upelelezi umeshakamilika hivyo atapelekwa mahakamani, watoto hawa walikuwa wakifanyiwa hivyo kwa nyakati tofauti” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Bukumbi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema mtoto huyo amekamatwa baada ya ofisa Mtendaji wa Kata ya Kihesa Kilolo, Elizabeth Lugenge kutoa taarifa ya kuwepo kwa watoto watatu wanaosoma katika shule ya Msingi Igeleke kulawitiwa

Kamanda huyo amesema taarifa zilifika kwa mtendaji lakini Wazazi wa wahanga hao walikuwa hawajui, ambapo amehoji kuwa ‘Wazazi wanakwama wapi’ kutofaham vitendo wanavyotendewa, ambavyo amedai vinatokea mara kwa mara.