February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MTOTO WA MIAKA 13 AOKOLEWA AKITUMIKISHWA KAZI ZA NDANI MWANZA


Warning: file_get_contents(https://www.youtube.com/get_video_info?video_id=-IvyKch2Mvk): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.0 410 Gone in /home1/watetezi/public_html/wp-content/themes/watetezi/inc/template-functions.php on line 834

MTOTO WA MIAKA KUMI NA TATU AOKOLEWA AKITUMIKISHWA KAZI ZA NDANI MWANZA

MTOTO WA MIAKA KUMI NA TATU AOKOLEWA AKITUMIKISHWA KAZI ZA NDANI MWANZA

Mtoto mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa mkoa wa Kigoma ameokolewa jijini Mwanza alipokuwa akitumikishwa kazi za ndani, inadaiwa binti huyo alikatishwa masomo baada ya wazazi wake kudai hawana fedha za kumsomesha na kisha kumsafirisha hadi mkoani Mwanza ambako anafanya kazi za ndani bila malipo, Watetezi TV ilipata taarifa za uwepo wa tukio hili na kufunga safari moja kwa moja hadi anapoishi binti huyo na kutaka kubaini ukwelii wa mambo.

Wakati natolewa nyumbani niliambiwa kwa kuwa umekaa nyumbani husomi na mama yako anashindwa kukununulia vifaa vya shule twende ukafanye kazi Mwanza, lakini alisema atanisaidia kwanza nisome nikuekue ndio nitaanza kufanya kazi” anaeleza mtoto huyo Mhanga wa utumikishwaji kazi za ndani na kudai kuwa alipofika tu jijini Mwanza kazi ikaanza rasmi bila kutimiza ahadi ya kupelekwa shule.

Hata hivyo mtoto huyu aliyetolewa Kigoma akiwa darasa la 4 anaeleza kuwa baadhi ya majukumu aliyoambiwa yalikuwa ni kuosha vyombo pamoja na kuwa mwangalizi wa mtoto pamoja na kupika chai, lakini baada ya mama aliyekuwa akiishi hapo kupata msiba na kuondoka na Watoto kubaki na baba yao kazi za binti huyu zikabadilika na kuanza kufanya kazi ngumu Zaidi ya mwanzo ikiwemo kumfulia baba mwenye nyumba nguo.

 Baada ya uwepo wa kazi numu bila malipo mtoto huyu alionelea nivema akianza kudokoa fedha kidogo katika kila senti aliyopatiwa kwa ajili ya matuizi a nyumbani ili apate baadhi  ya mahitaji yake binafsi ikiwemo mavazi, kwa kuwa hakukuwa na anayejali kuhusu yeye.

“Wenyewe waliponichukuwa kule waliniambia wataninunulia nguo na viatu nitakapofika huku, lakini baada ya kufika hawakuninunulia chochote, nilikuwa navaa viatu na nguo chache nilizokuja nazo” Mhanga.

Wakala bubu anayefahamika kwa jina moja la mama Abduli ndiye aliyehusika kumsafirisha msichana huyo mwenye ndoto za kuwa mwalimu na mpaka sasa hajulikani alipo huku wanaomtumikisha mtoto huyo wakitaka kumaliza swala hilo kimya kimya.

Watetezi TV iliamua kumtafuta Mwanaharakati wa masuala ya Watoto anayeshughulika na kesi hii na hapa mwanaharakati huyu Bi. Aisha Mtumwa anaeleza hatua alizochukua baada ya kusikia tetesi za tukio la kutumikishwa kwa mtoto huyo.

“Kitendo kile hakikunipendeza  nilimfata mama mwenye nyumba na kumtaka kutofumbia macho vitendo vya utumikishwaji wa Watoto, ambao wenzake wanakwenda shule na wao wapo wanatumikishwa kazi za ndani, afadhali wangepelekwa shule na pindi wakirudi waendelee na majukumu ya nyumbani” Bi Aisha Mtumwa, Mwanaharakati wa masuala ya Watoto akielezea kisa cha mtoto huyu aliyekuwa akitumikishwa kazi za ndani jijini Mwanza.

Bi Aisha anakiri kutojibiwa majibu ya kuridhisha na waliokuwa wakimtumikisha mtoto huyo na kuchukua hatua kwa kushirikiana na Dawati la ustawi wa Jamii pamoja na polisi ili kuwataka waajiri hao kulipa gharama za usafiri ili mtoto huyo asafirishwe hadi nyumbani kwao atakapotafutiwa shule na kusoma huku akiwataka waajiri hao kulipa mshahara wa miezi 8 kwa mtoto huyo aliyekuwa akifanyishwa kazi bila malipo.

Katika Mahojiano na Watetezi TV Daktari Peter John kutoka zahanati ya Usumao Iliyopo jijini Mwanza anawalaumu wazazi na jamii kwa kutoajibika kumlinda mtoto.

“Wazazi wengi bado hawajapata elimu muhimu kuhusu athari za Watoto katika malezi, hasa hasa Watoto wa kike, maana hapa tunapambana na watoto wenye umri mdogo sana wakiwa wamejiingiza kwenye uraibu wa madawa ya kulevya, wengine kufanyiwa ukatili wakati wanatumikishwa katika kazi za ndani” Dkt. Peter John

Pamoja na maswahibu aliyoyapitia binti huyu anasisitiza kuwa matamanio yake ni kuendelea kusoma kwani utumikishwaji wa kazi za ndani umemrudisha nyuma, na kutaja kuumizwa na kitendo cha kuwaona Watoto wenzake wakienda shule nayeye kubakia nyumbani kupambana na kazi za ndani.

“Mimi nilikuwa sifurahii maana Watoto niliokuwa nakaa nao walikuwa wanasoma na wanaenda shule wananiacha mimi ndani na kazi nilikuwa najisikia vibaya sana, sasa hivi nimeanzishwa memkwa darasa la tatu wasingenkatisha masomo sasa hivi ningekuwa darasa la tano” Mhanga wa utumikishwaji wa kazi za Ndani jijini Mwanza.

Mpaka sasa Kesi ipo katika kituo cha kati jijini Mwanza huku Mwanaharakati wa Watoto Bi. Aisha mtumwa akiahidi kuendelea kusimamia kesi hii hadi ifike mahakamani, na Watetezi TV itaendelea kuhabarisha kuhusiana na kisa hiki hadi tamati yake.

“Tunazidi kukandamiza kinamama wa baadae, hatuhitaji kuwa na kina mama wa baadae wasiokuwa na elimu tunahitaji kuliacha hili taifa kwenye mikono salama ambapo kina mama wanaokuja tutawatengenezea mazingira waweze nao kuwa kina mama bora kama tulivyo sisi sasa, tunapowadidimiza Watoto wa kike tunakuwa tunawapoteza kina mama wa baadaye, mwisho wa siku anakuletea Watoto wasiotarajiwa na hata magonjwa kwa kuwa hana elimu hatokuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo” Bi Aisha Mtumwa Mwanaharakati wa Maswala ya Watoto.