February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MSIMU WA KINA MAMA UONGOZINI? Anne Kananu Kuapishwa Gavana wa Nairobi

Na Dennis Chisaka,Nairobi Kenya

Kumekuwa na mvutano katika uongozi wa kaunti 047 ya Nairobi Kenya kwa muda sasa tangu aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi sonko kuondolewa mamlakani kutokana na kesi za utumizi mbaya wa afisi na ufisadi zilizokuwa zikimuandama. Kulingana na Kifungu cha 180 (2) cha Katiba ya Kenya, 2010. naibu gavana atachukuwa hatamu za uongozi moja kwa moja iwapo gavana atajiuzulu, kuondolewa madarakani au kufariki.

Ikumbukwe kuwa sonko hakuwa na gavana tangu mwaka 2018 baada ya aliyekuwa naibu wake Pollycap Igathe kujiuzulu, na alikuwa akiendesha shugli za kaunti bila msaidizi hadi kufikia wakati anaondolewa madarakani mwaka 2010.

Kabla ya sonko kuondoka afisini aliwahi kuteua majina tofauti ya watu aliowataka kuchukuwa nafasi ya naibu gavana, akiwemo Miguna miguna na Anne kananu, lakini jina la miguna likakataliwa kabla ya uteuzi kuendelea, hii ikampa Anne nafasi ila kufikia sonko anaondoka, jina la Anne halikuwa limepitishwa.

Picha : Polycarp Igathe akijiuzulu

Hii leo Mahakama Kuu imemteua jaji atakayesimamia hafla ya kuapishwa kwa Ann Kananu kama Gavana wa Nairobi mnamo Jumanne tarehe 16 nov 2021.

Katika barua iliyotumwa Jumatatu, Baraza Kuu Muciimi Mbaka alithibitisha kuwa jaji aliteuliwa kuongoza kuapishwa kwa kiongozi mpya wa kaunti ya Nairobi.

“Nimeagizwa na Mheshimiwa Jaji Mkuu kuwataarifu kuwa jaji ameteuliwa kuongoza hafla ya kuapishwa Novemba 16 saa 10 alfajiri,” Mbaka alisema.

Mbaka alipeleka barua kwa katibu wa kaunti.

Wakati huo huo, notisi ya gazeti la serikali imetolewa kabla ya hafla ya Jumanne.