February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MRITHI WA NDUGAI KUJULIKANA KESHO

Katibu wa Bunge,Nenelwa Mwihambi amesema hadi kufikia leo jioni wamepokea jumla ya majina tisa ya watakaogombea nafasi ya uspika.

Amesema majina hayo yaliwasilishwa na kukidhi matakwa ya kisheria katika uchaguzi wa spika unaotarajiwa kufanyika hapo kesho.

Wanaogombea nafasi hiyi ni Mohamed Said (NRA),Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP) ,David Daudi Mwaijojele (CCK),Georges Gabriel Bussungu(ADA-TEA),Kunje Ngombare Mwiru (SAU),Maimuna Said Kassim (ADC),Ndonge Said Ndonge(AAFP),Saidoun Abrahamani Khatib (DP) na Dkt Tulia Akson.

Kati ya wagombea hao nane sio wabunge na mmoja ni mbunge.