Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Watetezi za Binadamu Nchini Tanzania, (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tokea aingie madarakani amefanya kazi nzuri katika upande wa Haki za Binadamu ndani na Kimataifa.
“Kazi yako katika eneo la haki za binadamu ni kubwa sana na inaonekana kote Tanzania na duniani, taarifa rasmi kuhusu mchango wako katika kulinda na kueneza haki za binadamu kwa kipindi cha mwaka mmoja imeandaliwa kwa lengo la kutambua na kuweka kumbukumbu kwa mambo uliyofanya” amesema Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa.

Olengurumwa amesema kuwa Watetezi wa Haki za Binadamu ni wasaidizi wa Rais katika eneo la utetezi wa Haki za Binadamu.
“Watetezi wa haki za binadamu ni wasaidizi wako kama alivyo Makalla (Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam), katika masuala ya utawala na sisi hapa ni wawakilishi wako katika eneo la utetezi wa haki za binadamu” amesema Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa.
Mratibu huyo ameyasema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya THRDC.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA