March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MKUU WA WILAYA YA HANDENI, SIRIEL MCHEMBE ASIKITISHWA NA TUKIO LA MWANAFUNZI WA MIAKA 10 ‘KUBAKWA’

Na: Anthony Rwekaza

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe, amesikitiahwa na tukio la kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Malick Apolonary(20) kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10 anayesoma darasa la nne katika shule ya msingi Chanika Wilayani Handeni.

Akizungumza mara baada ya kufika sehemu tukio hilo na kukutana mtoto anayedaiwa kutendewa tukio hilo, Mkuu huyo wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe amesema tukio hilo ni la wazi, kwa kuwa mtuhumiwa amekamatwa akiwa sehemu ya tukio hilo”

“Tukio la kijana Malick aliyekutwa akimbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10, ni tukio la wazi, ushahidi upo na amekamatwa eneo la tukio” amesema Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe

Pia Siriel Mchembe amesema ameumizwa na tukio hilo ambalo limeonekana kuwasikitisha watu, na kupelekea kutokwa na machozi akidai licha ya cheo chake yeye kama Mama tukio hilo limemuumiza na amesema hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan jambo hilo litamuumiza.

“Jambo hili limeniumiza kama mama na kama Mkuu wa Wilaya, na hata Rais Samia Samia Suluhu Hassan jambo hili litamuumiza pia” Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza vyombo vya dola kumchulia haraka hatua za kisheria mtuhumiwa huyo ambaye tayari yupo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Watetezi TV, inaikumbusha Jamii kuwa Sheria za Tanzania kosa la ubakaji ni kosa la jinai pale mahakama inapotoa hukumu kwa mtuhumiwa kutenda kosa hilo adhabu yake inaagukia kwenye adhabu za kijinai kulingana na kosa ambalo Mahakama imejilizisha kutendewa na mtuhumiwa.

Vilevile katika kulinda haki ya kila mtoto wa kike kupata elimu sheria za Tanzania zimekuwa na meno makali kwa watuhumiwa wanabainika kushiriki mapenzi na hasa kuwapa ujauzito wanafunzi wa elimu ya msingi na Sekondari, kwa kuwa sheria za Tanzania zinazuia mwanafunzi aliyepata mimba kutoendelea na masomo kupitia mfumo wa kawaida.