March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MKUTANO WA WADAU WA KUPITIA NA KUKUSANYA MAONI KUHUSU SHERIA YA KUZUIA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI YA ZANZIBAR

Na Loveness Muhagazi

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania kupitia tawi lake la Zanzibar (THRDC-Zanzibar), na Chama cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali Visiwani Zanzibar (ANGOZA), Kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Marekebisho ya Sheria ya Zanzibar imeandaa Mkutano wa wadau wa kupitia na kukusanya maoni kuhusu Sheria ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi visiwani Zanzibar namba 1 ya mwaka 2012.

Mkutano huo unaofanyika leo Desemba 18, 2021 katika hotel ya Golden Tulip uwanja wa ndege umewahusisha wadau mbali mbali ikiwemo, Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, Tume ya Kurekebisha Sheria-Zanzibar, wanasheria mbali mbali,Pamoja na wadau wa Asasi za Kiraia visiwani humo kwa lengo la kujadili kwa kina sheria ya kuzuia rushwa na Uhujumu uchumi visiwani Zanzibar pamoja na kuangalia uwezekano wa maboresho katika maeneo kadhaa.

Pamoja na hayo washiriki wa mkutano huu wanatarajia kuangalia na kujifunza uzoefu wa nchi mbali mbali duniani katika kupambana na vitendo vya Rushwa na Uhujumu uchumi na namna Zanzibar inaweza kujifunza na kuboresha sheria hiyo kwa kutafuta mbinu mbadala, bora zaidi na zinazozingatia misingi ya haki za binadamu katika kupambana na vitendo vya Rushwa visiwani humo.

Hatua hii ni mwendelezo wa juhudi zilizoanzishwa na Mtandao wa watetetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC-Zanzibar) kwa kushirikiana na mamlaka mbali mbali katika Serikali ya mapinduzi ya Zanizibar ili kuhakikisha kunakuwa na maboresho ya sheria mbali mbali Pamoja na uzingatiwaji wa haki za binadamu katika Nyanja zote.

TRANSLATION…

STAKEHOLDERS’ LAW REVIEW WORKSHOP ON ZANZIBAR ANTI- CORRUPTION AND ECONOMIC CRIMES ACT

The The Tanzania Human Rights Defenders Coalition through its Zanzibar branch (THRDC-Zanzibar), Zanzibar Association of Non-Governmental Organizations (ANGOZA), in collaboration with the Revolutionary Government of Zanzibar through the Zanzibar Law Reform Commission and Zanzibar Anti- Corruption Bureau have jointly organized a Law review session for collection views on the Zanzibar Anti-Corruption and Economic crimes Act No. 1 of 2021.

The workshop , which is being held today, December 18, 2021, at Golden Tulip Hotel, brought together various stakeholders including the Zanzibar Anti-Corruption and Economic Corruption Authority, the Zanzibar Law Reform Commission, various lawyers, and civil society Organization’s stakeholders. This workshop provide a room for collective review of the corruption laws in Zanzibar and document potential areas of improvements.

Moreover , the participants will have time to learn best practices from other countries around the world on how they fight against corruption and economic crimes. The idea is to modernize Zanzibar anti-corruption strategies to suit the needs of society and integration of human rights based approaches given the fact that corruption is the cross border crime.

This initiative is a continuation of the efforts launched by the Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC-Zanzibar) in collaboration with various authorities in the Revolutionary Government of Zanzibar to ensure there is improvement in various laws for crime prevention and human rights adherence in all aspects of life.