December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MKINZANO WA KIMTAZAMO KWENYE SAKATA LA NGORONGORO ISIWE CHANZO CHA PROPAGANDA HASI

Na: Mwandishi wetu

Ni takribani zaidi ya miezi mitatu tokea sakata la Ngorongoro lilipoibuka na kupelekea kuwa mjadala mkubwa Nchini Tanzania mpaka linapoandikwa andiko ili Sakata hilo tayari limebisha hodi kwenye uso wa Dunia, Dunia inajua nini kinaedelea.

Sakata lenyewe linatokana kudaiwa kuwa awali Serikali ya Tanzania ilikuwa na nia ya kuwaondoa wananchi wanaoishi kwenye hifadhi ya Ngorongoro ambayo inatambuliwa katika maajabu saba ya Dunia, kuwaamishia kwenye maeneo mengine kwa madai ya kutaka kuinusuru hifadhi hiyo ikidaiwa watu n wameongezeka pamoja na mifugo ikilinganishwa na awali, licha ya madai hayo kuonekana siyo ya kitafiti hisipokuwa ilionekana kama makisio binafsi kutoka na takwimu kukindhana baina ya baadhi ya wahusika waliopata nafasi ya kuliezea jambo hilo.

Baada ya kuibuka kwa sakata hilo wadau mbalimbali walianza kulivalia njuga jambo hilo, ikiwemo Wanasiasa, Wanaharakati pamoja na mashirika mbalimbali yanaotetea haki za binadamu ikiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Haki Aridhi, PINGOs Forum na mashirika mengine ambayo yamekuwa yakitoa matamko na ushauri kwa Serikali juu ya hatua za kutatua mgogoro huo bila yasiyoathiri upande wowote.

Licha ya mitazamo hiyo kuonekana kuwa kindhani juu ya sakata hilo, imeonekana limezaa pande mbili, huku upande mmoja amabao unajivika koti la Serikali (kwa hoja ya maslahi mapana ya Taifa) likitaka wananchi hao waondolewe kwa ulazima licha ya Serikali kuweka hadharani msimamo wake kuwa mchakato huo unaratibiwa kwa uhiari ya wahusika wenyewe wanotaka kuama bila kulazimishwa.

Kundi la pili limekuwa likisisitiza sakata hilo kuheshimu haki za binadamu kwa jamii hiyo ya kimasai pia kuzingatia sheria, desturi na kanuni zinazoongoza au kuratibu uwepo wa jamii kwenye hifadhi ya Ngorongoro ambayo kihistoria imekuwepo kabla hata ya Tanganyika kupata uhuru, amabapo jamii hiyo iliamishiwa Ngorongoro kutoka Serengeti mnamo mwaka 1959 chini ya Serikali ya Kikoloni.

Utofauti huo wa kimtazamo umelifanya kundi linalodai kusimamia maslahi mapana ya Taifa, kutumia propaganda hasi zinazoweza kuchafua taswira ya jamii ya kimasai kwenye uso wa umma. Kuna mambo ambayo yanatakiwa kutekelezwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kama wajibu wa kisheria, mfano kuratibu zoezi la kutoa chakula, huduma za afya kwa jamii hiyo na huduma nyinginezo, lakini imekuwepo propaganda kutoka kwenye kurasa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya magazeti kuwa Jamii hizo zina ufukara wa kujitakia ikiwemo kuonyesha baadhi ya picha za jamii hiyo.

Pia zimekuwepo propaganda za kupotosha ukweli, na ikumbukwe sakata ili baada ya kuonekana kuibuliwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwataka wananchi kuepuka taarifa za kupotosha, propaganda hizo kueleza mambo ya upande mmoja kuhusu jamii ya Ngorongoro bila kutoa mwanya kwa jamii hizo kujibu madai yanayoelekezwa kwao, mfano kuhusu kuwa jamii hiyo haipati chakula cha kutosha hali ambayo inadaiwa kuwa inapelekea udumavu kwao.

Je, Wananchi hao wanapewa nafasi ya kueleza ni kwanini hawapati chakula cha kutosha au maitaji mengine ya kijamii?, Habari ikikosa usawa hiyo sio habari inaweza kuwa propaganda hasi.

Inapofikia wakati inaenezwa propaganda kuwa jamii ya kimasai inayoishi kwenye hifadhi Ngorongoro ni watu waliotokea Nchi Sudani na Kenya, sio jambo lenye afya kwa diplomasia baina ya Nchi ya Tanzania na hizo zinazohusishwa, lakini pia madai hayo yanatolewa bila uthibitisho wowote kutoka kwenye vyombo vya dola ikiwemo Jeshi la Uhamiaji.

Aidha pia Watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na wanaharakati wengine wenye mtazamo kindhani nao wamejikuta kwenye myororo wa kufanyiwa propaganda hasi, mfano wengine wamekuwa wakituhumiwa kuwa wanatumiwa na Nchi jirani hata wahisani ikidaiwa ni kwa lengo la kufanya hifadhi hiyo kupoteza hadhi iliyonayo kwa sasa.

Aidha pia Watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na wanaharakati wengine wenye mtazamo kinzani au wakawa tofauti na kile kinachoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari wamejikuta wakiingizwa katika mnyororo huo na kuchongewa propaganda zenye mitazamo kinzani mfano wengine wanatuhumiwa kufadhili wananchi wa Ngorongoro ili kusimama kinyume na Serikali yao na hata wengine wakituhumiwa kukimbilia nchi jirani, wahusika wanatakiwa kujilidhisha kabla mambo hayo hayajachapishwa au kuenezwa kwa umma ili kujiridhisha kupata ukweli halisi.

Ni muhimu kutafakari, Je, kazi ya watetezi wa haki za binadamu ni zipi? hawapaswi kuzungumza au kukemea pale panapoonekana kuna uvunjifu wa haki za binadamu?,Uhuru wa kujieleza upo wapi?. Kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha makundi yote yanapewa haki sawa ili waweze kutoa mitazamo yao inayoweza kuwezeshwa utatuzi wa kudumu wa mgogoro huo, lakini endapo katika shuguli zao za utetezi wanavunja sheria na taratibu za Nchi na kuna ushahidi wa jambo hilo, ni vyema tuhuma hizo kufikishwa kwenye vyombo vya dola ili wahusika wachukuliwe bila kuvunja sheria.

Kuna muhimu hoja za makundi yote kujibiwa kwa hoja sio kwa propaganda ambazo zinaweza kuleta taswira hasi, kama zipo takwimu au taarifa za kiuchunguzi zinaweza kuwekwa adharani ili kusaidia Wananchi kufahamu ukweli halisi wa sakata zima, Utetezi wa Haki za Binadamu sio jukumu haramu au kuwa wanaotetea jamii ya Ngorongoro ibakie kwenye hifadhi kuwa hawaoni maslahi ya Taifa.

NINI KIFANYIKE KUEPUKA PROPAGANDA HASI

Ni muhimu pande zote kutambua kuwa mkindhano wa kimtazamo sio jambo ambalo linatakiwa kuzaa propaganda hasi zisizo na tija kwa Taifa. Kunatakiwa kuwepo na mzani sawa kwa pande zote maoni yao kuheshimiwa ili mamlaka za kimaamuzi ambazo msingi wake ni wananchi ziweze kutoa uamuzi usiozingatia maengemeo ya upande mmoja, kama ni wananchi na ni muhimu kuendelea kupewa fursa ya kusikilizwa kama ambayo Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza.

Pia wadau pande zote mbili kwa kuzingatia hoja zisizovuja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria nyingine za Nchi, sio busara kunyosheana vidole au kujenga chuki wala kusakama mtu kisa utofauti kimtazamo, pande zote mbili ziwe na uwanja sawa wa kuwasilisha maoni kwa manufaa ya ustawi wa Hifadhi ya Ngorongoro.

Kuheshimu Sheria za Nchi hususani zinazogusa haki za binadamu, sio jambo jema kutumia propaganda zinazoweza kukihuka haki muhimu za watu mfano, kujenga kashfa kwa kundi ambalo lina mtazamo kindhani, kutokutuhumu Nchi nyingine kuhusika na sakata hilo bila tafiti wala uchunguzi wowote, kuna umuhimu wa kuheshimu diplomasia iliyopo baina ya Tanzania na Nchi jirani zinazohusishwa kwenye sakata hilo kwa kuwa Nchi hizoutegemeana na Tanzania kwa mambo mengi.

Propaganda hasi zisiingilie uhuru wa watu kutoa maoni yao, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaheshimu uhuru wa watu kutoa maoni yao bila kukiuka sheria na taratibu za Nchi, inapotokea inasambazwa taarifa ambayo aina maoni halisi ya jamii inayotuhumiwa ni kuikosesha haki yake ya msingi jamii hiyo.

Pia mihiko ya tasnia ya habari inatoa mwongozo kwa vyombo vya habari kuheshimu maadili ya kitaluma katika kuripoti habari, mfano mpaka taarifa iweze kuchapishwa kwenye chombo cha habari, inatakiwa kuwa ina ukweli, usahihi, usawa (Truth, Accuracy, Balance), ni muhimu hilo kuzingatiwa ili kuepuka madhara.

Kuepuka Propaganda hasi zinazoingilia uhuru wa vyombo vya ulinzi na usalama, Tanzania kuna vyombo vya kushughulikia tuhuma zinazohusu ukiukwaji wa sheria, inapotokea inaripotiwa taarifa yenye tuhuma inatakiwa kudhibitishwa kisheria na vyombo vinavyohusika kisheria, endapo propaganda hasi juu ya sakata la Ngorongoro zikiachwa zikaingilia vyombo hivi zinaweza kupelekea jamii kuwa na mtazamo hasi juu ya vyombo hivyo ambavyo ni nguzo ya amani na haki ndani ya Nchi.

Mkinzano wa mitazamo inayozingatia utu na mihiko ya kisheria iwe chachu ya kujenga desturi ya upembuzi hoja chanya zinazoweza kulisaidia Taifa kupata suluhu ya kudumu juu ya mgogoro huo ambao uibuka kwa mara kadhaa kwa zaidi ya miongo miwili, lakini utofauti huo usiwe kichocheo cha kuzaa uhasama wa kisiasa hata kijamii au kukiuka utu wa wahusika ikiwemo jamii hiyo ya kimasai.

Hata hivyo mbali hayo itakumbukuwa Serikali kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro ameweka wazi kuwa Serikali itazingatia haki za binadamu na imeruhusu demokrasia ikiwa ni pamoja na kuruhusu uwepo wa mijadala juu ya sakata la Ngorongoro na kuwa imekuwa ikifuatilia mijadala hiyo.

Hoja ijibiwe kwa hoja!Utofauti wa mitizamo kuhusu Ngorongoro isiwe chanzo cha uhasama na kuchapisha Propaganda zenye lengo la kuchochea uhasama juu ya kundi au watu fulani.