February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

“MIUNDOMBINU YA MASOKO NA MIFUMO YA UMEME NI YA ZAMANI” INJINIA MAJOBHELA

Siku chache mara baada ya kuungua moto soko la Karume jijini Dar es salaam, Injinia Ally Majobhela amesema miundombinu mibovu na mifumo ya zamani ya umeme ambayo haina marekebisho ni baadhi ya chanzo cha majanga ya moto yanayotokea nchini  katika masoko mbalimbali.

Hatua hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa matukio Moto kuzidi kushuhudiwa nchini Tanzania ambapo mwaka 2021 Watu 32 walipoteza Maisha na wengine 145 kujeruhiwa katika matukio ya moto 1803 yaliyotokea kati ya Januari hadi Desemba 2021.

Kauli hiyo ilitolewa na  Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi  Januari 5,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya matukio kwa mwaka ulioishia Desemba 2021.

Sio mara ya kwanza tukio la Moto kutokea katika soko la Karume ambapo itakumbukwa mwezi Januari mwaka huu soko hilo lililoungua huku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makalla akibainisha chanzo cha moto huo baada ya uchunguzi kufanyika kuwa ni kutokana na Mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za Kulevya.

Hali hii imekuwa ikiibua maswali mengi kwa wananchi juu miundombinu  na mifumo ya umeme katika masoko na kuona kuna haja serikali kufanyia marekebisho ya mifumo hayo.

Akizungumza suala hilo Injinia Ally Majobhela amesema miundombinu mingi katika masoko haina mifumo ya udhibiti wa majanga ya moto.

“Chanzo kikubwa ni miundombinu ukiangalia mifumo mingi ya masoko haina mifumo ya uzimaji moto” amesema Injinia Majobhela.

Hata hivyo ameongeza kuwa mifumo ya zamani kwenye masoko isiyofanyiwa maboresho, uvutaji sigara na usimizi mbovu imekuwa ikisababisha moto katika baadhi ya masoko.

Nae msanifu wa majengo kutoka jijini Mwanza Faithbeth Mkenda ametoa wito kwa serikali na jamii kwa ujumla kabla ya kuanza ujenzi wa masoko waangalie shughuli zinazolizunguka eneo hilo ili kupunguza majanga hayo.

“Mazingira yanayozunguka yataamua soko litakaaje, malighafi zitakazo tumika katika ujenzi na kujua ni kwa namna gani wanaweza kukabiliana na majanga mengine Kama mafuriko”, amesema Mkenda.

Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa Masoko kuungua Moto katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania Kama vile soko la Kariakoo, Karume na rangi tatu yote ya Dar es Salaam, Mlango mmoja jjijini Mwanza na soko la Sido Jijin

Akizungumza wakati wa Kikao kazi cha kuratibu

 

Kuungua kwa masoko haya kumesababisha hasara kwa wafanyabiashara kutokana na kupoteza mali na kusababisha kurudi nyuma kimaendeleo.