March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MILIPUKO YAIBUA TAHARUKI UGANDA, SHUGHULI ZASITISHWA KWA MUDA

Na: Anthony Rwekaza

Leo Jumanne asubuhi Novemba 16, 2021 hali ya taharuki imeibuka Nchini Uganda kwenye Jiji la Kampala, kufuatia milipuko miwili ya mabomu inayodaiwa kutokea kwa wakati mmoja katika maeneo mawili tofauti yanayolizunguka Jiji hilo.

Katika hali ya sintofahamu Wananchi wameonekana kuyakimbia maeneo yao ya biashara na makazi kutokana na moto ulioambatana na moshi mkali kutanda kwenye maeneo yalipotokea matukio hayo yaliyozua gumzo.

Kufuatia tukio hilo kwa mujibu wa tovuti ya Daily Monitor, inadaiwa mlipuko wa kwanza umetokea karibu na kituo Kikuu cha Polisi na huku mlipuko wa pili ukitokea karibu na jengo la ukumbi wa Bunge la nchi hiyo.

Inaelezwa na vyanzo mbalimbali vya taarifa kuwa Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa na milipuko hiyo iliyoacha na kusababisha uharibufu mkubwa wa mali na magari kutokana na moto uliotanda kwa muda mrefu huku mamlaka za zimamoto zikipambana kuuzima.

Licha ya uharibifu huo shughuli mbalimbali katika baadhi ya majengo yaliyopo karibu na kando na mlipuko huo ilipotokea kadhia hiyo zimestishwa kwa muda mpaka hali ya usalama itakapo imeimarishwa.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwa kwenye maeneo ilipotokea milipuko hiyo wanadai Majengo, ofisi na makazi yao yalitikisika wakati milipuko ulipotokea, ushuhuda huo umeelezwa na Vyombo mbalimbali ikiwemo BBC. Lakini mashuhuda wanadai walishudia magali yaliyopakiwa nje ya ofisi ya bima yakiungua.

Taarifa za awali hazijaeleza idadi ya majeruhi wala taarifa ya vifo, lakini kama itakumbukuwa Oktoba 2021 iliripotiwa kutokea milipuko miwili tofauti nchini Uganda, iliyodaiwa kusababisha vifo vya watu wawili.

Taarifa kutoka kwenye chombo cha habari cha BBC kilibainisha kuwa walifariki ni muhudumu katika baa na mwingine, mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alidaiwa alikuwa ameingiza vilipuzi kwenye basi.

Mamlaka nchini Uganda zimekuwa zikilishtumu kundi la waasi wa Kiislamu Allied Democratic Forces (ADF) lenye makao yake kwenye nchi tofauti ikiwemo Uganda, DR Congo linalodaiwa kuhusika na matendo kigaidi, kwa kuhusika na milipuko miwili iliyotokea Oktoba 2021, ambapo tayari watu takribani watu 50 wamekamatwa, na wengine kushtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusishwa matukio hayo.