February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MFALME MSWATI AKIMBIA NCHI

Mfalme Mswati wa Eswatini.

Na Leonard Mapuli.

Mfalme Mswati wa Eswatini (Zamani Swatzland)  amekimbia nchini kwake baada ya kuanza kwa maandamano  ya kudai mabadiliko ya kidemokrasia nchini humo huku akitoa maelekezo ya kukamatwa kwa wabunge Mduduzi Bacede Mabuza na Mduduzi ‘Magawugawu’ Simelane wanaodaiwa kuratibu maandamano hayo.

Kwa mujibu wa mwanasheria  wa masuala ya haki za binadamu,polisi wamekaidi kutii agizo la kuwakamata  kwa wabunge hao,lakini mfalme Mswati ameelekeza  jeshi la nchi hiyo  kutekeleza maagizo hayo.

“Mfalme Mswati ameagiza jeshi liwakamate wabunge wawili wanaongoza vuguvugu la kudai demokrasia,sasa lazima kwanza tuhakikishe usalama wao maana haijawahi kutokea jeshi kumkamata mwanasiasa yoyote” amesema mwanasheria huyo.

Mfalme Mswati ametoroka nchini kwake kwa kutumia ndege yake binafsi na kuacha nchi chini ya utawala wa kijeshi ambapo imeripotiwa kuwa askari walianza kufyatua risasi kuwatawanya watu waliokuwa wakishiki maandamano.Huenda maandamano hayo yakashika kasi zaidi leo (Jumanne)  na kushambulia mali za Mfalme Mswati na za serikali.

Jana (Jumatatu) baadhi ya maduka na magari yalichomwa moto katika mji wa Matsapha na maeneo mengine yenye yaliyotawaliwa vurugu.

Msemaji mkuu wa Mfalme Mswati amekataa kuzungumza chochote kila alipohojiwa  huku simu zote za mkononi za Mswati zikiwa hazipatikani.