February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MFAHAMU LUT. MAMADY DOUMBOUYA,ALIYEMPINDUA CONDE,NA KUTENGWA NA ECOWAS

Na Leonard Mapuli.

Jina Colonel Mamady Doumbouya,huenda limekuwa maarufu zaidi dunia kuanzia September 5,baada ya kumpindua madarakani,rais wake na amiri jeshi wake mkuu,Alpha Conde huko nchini Guinea.

Wawili hawa (Rais Conde na Doumbouya) wanatoka kabila moja la Maninka (Malinke,Mandinka,ama Mandingo),linalopatikana katika nchi karibu zote za Afrika Magharibi,ambalo ni kabila dogo linalotawala kabila kubwa la Fulani nchini Guinea.

Doumbouya,baba wa Watoto watatu,ana umri wa miaka 41 tu,lakini uzoefu wake jeshini ni miaka 15,akihudumu katika idara mbalimbali nyeti za ulinzi wa taifa la Guinea,lilojitwalia uhuru wake mwaka 1958,akihudumu katika idara  ujasussi na uchunguzi eneo la Magharibi mwa Guinea.

Elimu ya kijeshi ya Doumbouya haitii shaka kuwa alikuwa na uwezo wa kupindua nchi kwani amepata mafunzo ya nchini Israel,juu ya masuala ya ulinzi,Mafunzo ya Usimamizizi wa misheni za kijeshi aliyopatiwa nchini Gabon,Pamoja na mafunzo ya kikamanda,aliyopatiwa katika shule maalumu ya kijeshi nchini Senegari,na amepata mafunzo katika Chuo cha Vita cha nchini Ufaransa.

Kifupi ni mbabe wa mzoefu wa vita,hii ni baada ya kushiriki vita kadhaa ikiwemo kumuondoa rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast mwaka 2011,baada ya kuripotiwa uwepo wa uvunjwaji wa haki za binadamu kwa kiwango kikubwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.Alikuwa pia miongoni mwa waliotumwa kulinda amani nchini Djibout chini ya Umoja wa Mataifa baada wanamgambo wa Seleka kuwa katika vita kali na wanajeshi watiifu wa Rais François Bozizé mwaka 2013 kabla hajakimbia nchi,Doumbouya ameshiriki vita vya Afghanistan mwaka 2014 na amekuwa katika ulinzi wa vuongozi mashuhuri katika nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza,Cyprus,Israel,na baadae nchini kwake Guinea,kabla ya kutimkia Ufaransa ambako alihudumu kama mwanajeshi wa kigeni (Legionnaire),ambako pia inadaiwa aliutaka sana Uraia wa Ufaransa ili abaki nchini humo lakini haikuwezekana.

Rais Alpha Conde,aliyeingia madarakani mwaka 2010,tena kwa kuvunja rekodi katika uchaguzi unaodaiwa kuwa wa kwanza huru na wa haki,aligombea tena urais  mwaka 2015 kwa muhula wa pili kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo,na ilipofika mwaka 2018 (Miaka miwili kabla ya ukomo wa urais kikatiba nchini Mali),ndipo alipoamua kumtoa Komamdo huyu aliyekuwa nchini Ufaransa,na kumrejesha Guinea na kumpa kuongoza kikosi maalumu (Special Forces Group) cha Ulinzi wa jeshi nchini humo.

Conde alijua kaleta mtu mwenye kumsaidia tena kwa vile alikuwa ughaibuni,hawezi kuipinga kiu yake ya kujiongezea muda wa kuitawala Guinea,na kweli akafanikiwa kugombea tena urais wa nchi hiyo kinyume na katiba mwaka 2020,na kujitangaza mshindi wa kiti cha urais kwa asilimia 59 katika uchaguzi wa Oktoba ,matokeo ambayo yalizua machafuko nchini humo na maandamano yasiyokoma ya wananchi kupinga  kukanyagwa kwa katiba,ambapo watu kadhaa waliuawa katika maandamano wakikabiliana na polisi.

Mnamo September 5,aliyetolewa Ufaransa  mwaka 2018,pengine kumsaidia Conde kutawala kiulaini kinyume na katiba,kijana wa miaka 41, Mamady Doumbouya,alimuondoe Conde,mzee wa miaka 53 asiikalie Ikulu ya Guinea kwa maslahi yake na Rafiki zake wachache,bali Ikulu akae mtu mwenye maslahi na raia wa nchi hiyo,wapatao milioni 12.4.

Jumuiya mbalimbali za kimataifa zimelaani kitendo hicho,huku Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ikiivua uanachama Guinea kama hatua mojawapo kulaani mapinduzi yaliyofanywa na Doumbouya.