Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
Mbunge wa jimbo la Ngorongoro, Emmanuel Shangai pamoja na viongozi wa mila na baraza la wafugaji Ngorongoro,wametaka uwepo wa maridhiano ya pande zote katika kumalizia mgogoro wa matumizi ya ardhi baina yao na shughuli za utalii na uhifadhi.
Wakizungumza na watetezi TV, viongozi hao wameeleza shinikizo la kutaka kuwaondoa kwa nguvu katika maeneo yao ya asili haiwezi kuwa suluhu.
Shangai alisema kwa asili jamii yao ni ya uhifadhi hivyo propaganda za kuwahusisha na uharibifu wa mazingira ama matukio mengine ya kuathiri wanyama na misitu sio kweli.
“Sisi tupo tayari kukaa na serikali kujadiliana njia bora ya kuondoa changamoto zilizopo kwani sisi tunahaki sawa na watanzania wengine kuishi katika ardhi ya asili”alisema
Alisema kwa suala la hifadhi ya ngorongoro ni muhimu sheria iliyoanzisha hifadhi hiyo mwaka 1959 kufuatwa kubwa hifadhi imeanzishwa kuendeleza uhifadhi utalii na wenyeji wa ngorongoro.
“Sasa mkakati wowote kutaka kutuondoa ni kuvunja sheria na sisi hatuishi Ngorongoro kwa bahati mbaya kwani wazazi wetu waliondolewa Serengeti na kuhamishiwa Ngorongoro “alisema
Mwenyekiti wa viongozi wa mila Ngorongoro,Metui ole Shaudo alisema wao hawana ugomvi na serikali bali kuna watu wanataka kuwagombanisha kwa maslahi yao
” Sisi tumezaliwa hapa na hatutaondoka kwa nguvu Ngorongoro huu ni ardhi yetu na tunawapinga wanaochochea vurugu na kutoa taarifa za uongo”alisema
Mwenyekiti wa baraza la wafugaji Ngorongoro Edward Maura alisema wao ni wakazi halali wa ngorongoro na wanachonga is na Mamlaka ya hifadhi hiyo kuonekana sio wakazi halali ‘a wanavunja sheria.
” Sisi kwa sasa hatuna imani tena na uongozi wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ndio sababu kuanzia sasa tumegomea cha chai,dawa za mifugo na mahitaji mengine kwani hawana nia njema na sisi na wamefikia hatua kutupa chumvi feki ya mifugo ili ife”alisema
Alisema wanapinga hoja kubwa wao ni waharibifu wa mazingira na ni tishio kwa wanyama na utalii kwani wamekuwa Ngorongoro tangu kuanzishwa na kila mwaka watalii wanaongezeka.
Kutokana na mgogoro huu waziri mkuu Kassim Majaliwa tayari amekutana na wananchi wa loliondo kupokea maoni yao juu ya eneo la kilometa za mraba 1500 ambalo linapendekezwa kuhifadhi wa
Waziri mkuu pia atatembelea mamlaka ya hifadhi Ngorongoro na kupokea maoni ya wakazi ili baadaye serikali itoee maamuzi.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA