February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MBUNGE APELEKA MAPENDEKEZO YA NGO’S SERIKALINI.

Mbunge wa Viti Maalumu kutoka kundi la Asasi Zisizo za Serikali bungeni,Neema Lugangira,amekutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi maalumu Dkt. Zainabu Chaula,katika ofisi mpya za Wizara hiyo,eneo la Mtumba, jijini Dodoma,Jumatatu ya leo,Januari 24.

Mbunge huyo amefika katika Ofisi za Wizara hiyo ili kuwasilisha Mapendekezo kadhaa yanayohitaji kufanyiwa kazi ili kuongeza ukuaji na ufanisi wa utendaji kazi kwa Asasi Zisizo za Kiserikali kote nchini.

Miongoni mwa Mapendekezo yaliyowasilishwa ni pamoja na kuzijengea uwezo Asasi Zisizo za Kiserikali ziliko mikoani,kanuni ya usimamizi wa fedha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali,uondoa kodi kwa wafanyakazi wa kujitolea katika wanaofanya kazi katika mashirika, na usimamizi wa kodi.

Suala lingine walilojadili ni kuandaa Mikutano ya Kimkakati na Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika maeneo muhimu ikiwemo kuboresha Kanuni za Usimamizi wa Fedha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Dkt Chaula ameihakikishia Sekta ya Asasi Zisizo za Kiserikali kuwa,atashirikiana nayo kwa karibu ili kuimarisha umoja na kuweka Mazingira Wezeshi kwa Ustawi wa Sekta hiyo muhimu katika Maendeleo ya nchi.

Akizungumza na Watetezi TV kwa njia ya simu baada ya kukutana na katibu mkuu,mbunge Neema Lungangira amesema amefarijika sana kufikisha  Mapendekezo ya Asasi Zisizo za Kiserikali kwenye wizara husika,na kuongeza kuwa,endapo serikali itayafanyia kazi mapendekezo hayo itakuwa imechangia kwa kiasi kikubwa,ukuaji wa sekta ya NGOs nchini.

Aidha Neema amezitaka Asasi zote zisizo za Kiserikali,kuitumia vyema Wizara hiyo mpya,iliyomegwa kwa iliyokuwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watu wenye Mahitaji Maalumu kwani sasa ni wizara iliyopungunguziwa mzigo na ni rahisi kushughulikia changamoto zao kwa muda mfupi.

Mbunge wa Viti Maalumu kutoka kundi la Asasi Zisizo za Serikali bungeni,Neema Lugangira,amekutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi maalumu Dkt. Zainabu Chaula jijini Dodoma,Jumatatu ya leo,Januari 24.