February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MBUNGE AITAKA SERIKALI ILIVALIE NJUGA SUALA LA TAULO ZA KIKE

Mbunge wa Viti Maalumu Neema Rugangira ameitaka serikali kuja na mpango wa kuhakikisha mtoto wa kike hakosi kuudhuria masomo kwa sababu kukosa taulo za kike pindi anapokuwa kwenye hedhi.
Mbunge huyo amesema kutokana na tafiti ya NIMRI ya mwaka 2021 ilionyesha watoto wengi wa kike wanakosa shule kwa sababu yakuwa kwenye hedhi na moja ya sababu ni kukosa taulo za kike.
Lakini Mbunge huyo ameishauri Serikali kuwa inaweza kutumia mfuko wa TASAF katika mkakati wa kutatua changamoto hiyo ambapo amedai kuwa wahanga wengi wanatoka kwenye kaya maskini, pia amesisitiza juu ya suala la lishe kutolewa mashuleni ikiwa ni mwendelezo wa hoja ambayo amekuwa akiisemea mara kwa mara ndani na nje ya Bunge.