March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MBOWE NA WENZAKE 11 WAKAMATWA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa orodha ya majina 11 ya wanachama na viongozi wa chama hicho ambao walikamatwa na polisi hapo jana majira ya saa nane usiku wakiwa katika hoteli ya Kingdom waliyofikia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama hicho imesema viongozi 10 wamepelekwa katika kituo kikuu cha polisi Mwanza huku M/kiti wao,Freeman Mbowe mpaka sasa hajulikani alipo toka alipokamatwa na kulitaka jeshi la polisi kueleza sababu za kumkamata kiongozi huyo na kueleza wapui alipo.

Kutokana na sintofahamu hiyo Chama hicho kimelitaka Jeshi la Polisi kueleza sababu za kumkamatwa kwa kiongozi huyo na kueleza wapi alipo, aidha chama hicho kimelaani vikali tukio hilo.

Ikumbukwe kuwa CHADEMA ilipanga kufanya kongamano maalumu la kudai Katiba mpya Mkoani Mwanza kwenye hotel ya Tourist zamani ikitambulika (Tai 5).

Miongoni mwa wafuasi waliokamatwa ni

1.Freeman Mbowe

2. John Pambalu

3. John Heche

4. Rose Mayemba

5. Masenya (Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)

6. Steven Odipo

7. Dr Azavel Lwaitama

8. Seti (Dereva wa Kanda ya Victoria)

9. Apolinary Appolo (Afisa habari BAVICHA Taifa)

10.Frank Novatus (Chaso Mwanza)

11.Benjamin Kambarage (Mwenyekiti BAVICHA Kinondoni)