February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MBATIA AFUNGUA KESI KUPINGA MCHAKATO WA KUJIUZULU KWA NDUGAI

James Mbatia-M/Kiti NCCR Mageuzi

Na Hilder Ngatunga

Mwenyekiti wa chama cha NCCR –Mageuzi, James Mbatia amefungua kesi mahakamani akipinga mchakato wa  kujiuzulu kwa  aliyekuwa spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai  na pia anapinga utaratibu unaoendelea wa uteuzi wa spika mwingine  wa Bunge .

Shauri hilo namba 2/2022 limepitishwa chini ya hati ya dharura na limepangwa kusikilizwa siku ya Jumatatu mbele ya Jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu.Mbatia katika kesi hiyo atawakilishwa na mawakili Zaidi ya 10. Wengine wanaoshitakiw

Anasema Katiba imeweka utaratibu maalum wa kujiuzulu pale mtu anaposhikilia nafasi ya spika lakini katika mchakato wa kujiuzulu kwa Ndugai utaratibu huo uliwekwa kando hivyo unamfanya Ndugai kuemdelea kuwa Spika wa Bunge Kikatiba.

“Katiba imeeleza kuwa mtu akiwa kwenye nafasi ya uspika akitaka kujiuzulu ajiuzulu kwenye Bunge au Katibu wa Bunge lakini,utaratibu uliofuatwa na tukaelezwa umma wa watanzania kupitia Job Ndugai aliyesaini taarifa kupitia kwa wanahabari.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi anasema kwamba yeye ndio aliandikiwa na Katibu wa Bunge akapewa nakala ya kujiuzulu kwa Ndugai utaratibu huo ni batili na usiokubalika kikatiba,”amesema Mbatia.

Wakati hayo yakiendelea mchakato wa Kumpata mrithi wa Ndugai aliyejiuzulu Januari 6 mwaka huu unaendelelea,Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu CCM imemtangaza Dkt Tulia Akson kuwa mgombea wa uspika  na Chama cha ADC kimemtangaza Maimuna Said kupeperusha bendera ya chama hicho katika mtanange wa kumpata Spika wa Bunge.