February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA KAMBO

Na: Anthony Rwekaza

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga limemshikiria mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga (26) (jina limehifadhiwa), kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 11.

Akizungumzia taarifa hiyo kwa vyombo vya habari,April 11, 2022, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, George Kyando alisema tukio hilo limetokea juzi Aprili 9, 2022, saa 8:30 mchana.

Pia alisema mtuhumiwa alimnajisi mtoto huyo wakati mama yake akiwa ameenda dukani, na kisha kumsababishia maumivu sehemu zake za siri hali iliyopelekea kutokwa damu.

“Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga tunamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga kwa kosa la kumbaka (kumnajisi) mtoto wake wa kambo,” alisema Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga George Kyando.

Aidha katika taarifa yake amesema kuwa bado upelelezi tuhuma hizo unaendelea, na kwamba mtuhumiwa akikutwa na hatia atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Hata hivyo Kamanda huyo amewasisitiza Wananchi Mkoani Shinyanga kuachana na matendo maovu ya ukatili hususani ukali kwa watoto.

Ikumbukwe kwa mara tofauti Mkoa wa Shinyanga umekuwa miongoni mwa Mikoa ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwa na matukio tofauti ya ukatili hususani kwa watoto na wanawake licha ya Jeshi la Polisi pamoja Viongozi wa Serikali, taasisi zisizo za kiraia kuendelea kukemea matukio hayo pamoja na kuelimisha umma juu ya madhara yatokanayo na vitendo hivyo viovu.