March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAWAKILI WA MBOWE WAWASILISHA HOJA ZAO KUPINGA ‘DIARY’, MAHAKAMA KUMALIZA UTATA

Na: Anthony Rwekaza

Baada ya Mawakili wa utetezi kwenye kesi ndogo ndani ya kesi msingi namba 16/2021 inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake kuwasilisha hoja za kupinga kitendo cha shahidi wa pili wa Jamhuri kukutwa na ‘diary’, peni na simu akiwa kizimbani, Jaji Joachim Tiganga ameahirisha kesi hiyo mpaka kesho Novemba 16, 2021 saa 5:00 asubuhi ambapo atakuja kutolea uamuzi jambo hilo.

Katika hoja zao Mawakili wa utetezi waliiomba mahakama kumuondoa shahidi huyo na ushahidi wake kwa madai kuwa amekiuka sheria zinazomwongoza shahidi wakati akiwa kizimbani, leo wakati wakitoa hoja zao wameomba kuipitia kwa pamoja diary hiyo ambayo hipo mikononi mwa Mahakama, endapo upande wa Jamhuri watakuwa wanaamini yaliyomo kwenye diary hayahusiani na ushahidi.

Akijibu hoja za mawakili wa upande wa Jamhuri, Wakili Peter Kibatala ameambia Mahakama kuwa kwenye hoja zilizotoelewa na upande Jamhuri ili kuiwezesha Mahakama kutoa uamuzi hazikujikita kueleza au kikanusha kama vitu vinavyoweza kuwa kwenye diary havina uhusian na ushahidi uliotolewa na shahidi, bali hoja zao zimejikita kwenye mbinu za kumnusuru shahidi wao.

Awali mawakili wa Serikali walipopewa nafasi wamesema hoja za utetezi hazina mashiko ya kutosha kisheria hivyo wakaiomba Mahakama kutozipa msingi bali shahidi aendelee na hatua nyingine za ushahidi, huku wakifafanua kifungu cha 7 na 8 cha sheria inayomwongoza shahidi kuwa haijaelezwa kuwa shahidi hatakiwi kuwa na kitu chochote, jambo ambalo limepigwa na mawakili wa upande utetezi wakitaka Mahakama kurejea kwenye vifungu vingine kikiwemo kifungu cha 6, ambacho kinaelezea vitu ambavyo shahidi utakiwa kuwa navyo kwa ruhusa ya Mahakama.

Ikumbukwe Ijumaa Novemba 12, 2021 mawakili wa upande wa utetezi waliiambia Mahakama kuwa shahidi wa Jamhuri aliyejitamburisha kwa jina H4323 DC Msemwa anayo diary, peni na simu, ambapo shihidi alikili kuwa na vifaa hivyo, na alikabidhi diary hiyo Mahakamani baada ya mabishano ya hoja yaliyopelekea kesi hiyo kuahirishwa mpaka leo jumatatu Novemba 15, 2021.