February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAUAJI YAWAIBUA LHRC, WATAKA DESTURI YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI IKOME, WATOA USHAURI KWA WAPENZI

Kufuatia kuripotiwa kwa matukio mbalimbali juu mauaji yatokanayo na Watu kujichukulia sheria mkononi, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamesikitishwa na mwenendo wa matukio hayo, ambapo wameeleza kuwa katika kupindi cha mwezi Mei 2022 tayari wameripoti matukio sita (6).
Katika taarifa ambayo imetolewa kwenye tamko ambalo wamelitoa leo Jumatatu Mei 30, 2022 wamedai kuwa mauaji hayo yamekuwa yakitokana na wivu wa mapenzi.
Ambapo katika taarifa hiyo wameeleza kuwa matukio hayo yameshamiri zaidi kwenye Mikoa ya Arusha, Mbeya, Mara, Mwanza, Mara, Shinyanga na Manyara.
“Kwa mwezi Mei 2022 pekee, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeripoti zaidi ya matukio sita (6) yatokanayo na mauaji ya wivu wa mapenzi pamoja na tukio la hivi karibuni la wananchi kujichukulia sheria mkononi huku matukio hayo yakishamiri zaidi kwenye Mikoa ya Arusha Mbeya Mwanza, Mara, Shinyanga na Manyara” imeeleza hiyo ambayo imesainiwa na Mkurugezi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Ambapo wameeleza kuwa taarifa zinaonesha kuwa matukio hayo, kuwa matukio mengi yanatokana na wanandoa kwa sababu ya wivu wa kimapenzi, Lakini pia wametaja kuibuka kwa wingi kwa mauaji yanayotokana na wananchi wenye hasira kali kujichukulia sheria mkononi.
Aidha katika tamko hilo wameeleza kuwa licha ya Nchi kuwa na mifumo mizuri ya utoaji haki ikiwemo Jeshi la Polisi na Mahakama lakini kumekuwepo na utamaduni wa raia kujichukulia sheria mkononi wakitolea mfano visa vinavyotokea pale raia wanapowakamata watuhumiwa wa wizi, lakini wamesema kwenye tamko hilo kuwa hata licha ya sheria za Tanzania kuweka mifumo bora kwa wanandoa kuachana lakini visa matukio ya mauaji bado yameendelea kuwepo kwa wanandoa .
Hata hivyo wameishauri mbinu za kuchukua ili kuepusha matukio hayo, ambapo wamewataka Wananchi kuripoti matukio ya uharifu kwenye mamlaka za kisheria na sio kujichukulia sheria mkononi jambo ambalo ni kinyume na sheria zinavyoelekeza.
“Wananchi waripoti matukio ya uharifu kwenye vyombo vyenye mamlaka ya kuchukua sheria na sio kujichukulia sheria mkononi”imeeleza taarifa hiyo
Pia wamevishauri vyombo vya dola kurejesha imani kwa wanachi, ambapo wamesema kulingana na tafiti inaonesha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vimekuwa vikichagizwa na wananchi kukosa imani na vyombo hivyo.
Vilevile wametoa ushauri kwa wanandoa kufuata taratibu za sheria ya ndoa pindi wanapogubikwa na sintofahamu na sio kuchukua uamuzi wa kutoana uhai.
“Wanandoa kufuata utaratabu uliowekwa na sheria ya ndoa pindi wanaposhindwa kuelewana na sio kutwaa uhai wa mwenza”imeeleza taarifa hiyo
Lakini pia wamewataka wenza kuwa na desturi ya kutoa taarifa pale wanapofanyiwa ukatili na wenza wao ili kupatiwa msaada kwa lengo la kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
Ikumbukwe usiku wa kuamkia Mei 29, 2022 limeripotiwa tukio la mauaji mkoani Mwanza, ambapo mme anadaiwa kumuua Mke wake kwa kumpiga risasi, huku wivu wa mapenzi ukitajwa kuwa na kati ya sababu ambazo zimechagiza mauaji hayo.
-Endelea kufuatilia @watetezitv Kwa habari kemkem za kuhabarisha,kuelimisha na masuala ya haki za binadamu saa 24