February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAUAJI YA MTOTO ELISIE:MAMA WA KAMBO,MFANYAKAZI WA NDANI,MBARONI.

Marehemu Elisie Akeza Rutiyomba enzi za Uhai wake.

Polisi nchini Rwanda inawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuhusishwa na mauaji yam toto Elisie Akeza Rutiyomba,aliyeuawa na kisha kutumbukizwa katika tenki la maji,eneo la Busenza,Kijiji cha Kanombe,wilayani Kicukiro.

Kwa mujibu wa Polisi,Mama wa kambo wa mtoto huyo Pamoja na mfanyakazi wa nyumbani,ni miongoni mwa waliotiwa kizuizini na jeshi hilo kwa uchunguzi Zaidi.

Elisie,alipatikana akiwa amekufa,mwishoni mwa juma lililopita akidaiwa kutumbukia katika tenki la maji,mnamo Januari 14 mwaka huu.

Msemaji wa idara ya Upelelezi ya Rwanda,amewambia wandishi Habari kuwa uchunguzi wa kina unaendelea ili kutambua kama kuna watu walihusika kwa namna yoyote na mauaji ya mtoto huyo.

“Uchunguzi wa awali unaonesha Dhahiri kuwa watu wawili wanaweza kuhusika na mauaji ya yule mtoto,watu hawa nai Pamoja na mama wa kambo,Pamoja na mfanyakazi”,amesema msemaji wa idara ya Upelelezi.

Mpaka sasa watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Kanombe huku mwili wa mtoto huyo ukisalia katika maabara ya kimahakama chini Rwanda.