March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

JAJI MAKARAMBA AWAPA SHULE MAWAKILI ZANZIBAR

Jaji Mstaafu Robert Makaramba akizungumza na baadhi ya Mawakili wa Zanzibari.

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Robert Makaramba amesema mapungufu  ya Kikatiba yanalalamikiwa kuwemo katika Katiba ya Zanzibar na ile ya Tanzania Bara,ni mtokeo ya mfumo uliotumika wakati wa Uandikaji wa Katiba hizo.

Jaji Makaramba amesema hayo wakati wa mjadala ulioibuka baina ya mawakili wanohudhuria Mafunzo ya Siku ya mbili kuhusu Utetezi wa Haki za Binadamu visiwani Zanzibar,yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi Wa haki za Binadamu Tanzania,THRDC kwa ushirikiano na asasi nyingine za Zanzibar ikiwemo ZLSC,ZAFELA, na ZLS,ambapo Mawakili walitaka ufafanuzi juu masuala mbalimbali yanayotofautiana katika utekelezaji wake baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Katiba ni kanuni ambazo zimekuja kuashiria vitu ambavyo tayari viko kwenye jamii na ndio viko juu ya Katiba,ni kanuni za kuongoza jamii”,amerejea Jajii Makaramba aliporejea kanuni za Kijerumani zinavyotumika kutengeneza Katiba.

.Baadhi ya Mawakili wa Zanzibar wakimsikiliza kwa Makini Jaji Mstaaf Robert Makaramba

Kwa mujibu wa dhana nyingi duniani,Katiba inarejewa kama sheria mama ambazo hutungwa na binadamu,ambayo pia inaweza kupingwa na binadamu huyo huyo,jambo ambalo halitekeleki kwa Tanzania ambapo nguvu kubwa ipo chini ya bunge na si watu..

Uamuzi uliowahi kufanywa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania,ambayo ndio Mamlaka ya juu kabisa,umelipa Bunge la Jamhuri ya Tanzania kufanyia mabadiliko kifungu chochote ndani ya Katiba ili mradi imefuata utaratib uliowekwa kwa mujibu wa katiba.Utaratibu huu Tanzania iliiga kutoka nchini Indio ambako baadae ulibadilishwa na sasa nchi hiyo ili kubadili kifunuo chochote ndanu ya Katiba,ni lazima kurudi tena kwa wananchi.

“Mfano Tanzania tukitaka kugeuza mfumo wa vyama vingi kuwa wa Chama kimoja,hatuwezi kwenda Mahakamani,tutaenda kwa wananchi tuwaulize,bahati nzuri tulipoingia mfumo wa vyama vingi wananchi hawakuamua,ni rais wan chi ndio aliamua”,amesema Jaji Makaramba akielezea udhaifu wa kimfumo uliotumiwa kuandika katiba ya Tanzania,na ule uliotumika kuandika katiba ya Zanzibar kabla ya Mabadiliko,unavyotoa nafaso kwa masuala mengi kufanyika tofauti kati ya Zanzibar na Tanzania Bara na kwamba kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini siyo kila Mtanzania ni Mzambari kutoka na uwepo wa sheria ndani katika ya Zanzibar Jamhuri ya Muungano kuwa na masuala yasiyohusu Muungano.

Haki za Binadamu ni moja ya mambo mengine Muhimu katika katiba yoyote,lakini Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ni tofauti.Katiba ya Tanzania ya sasa Bunge la Tanzania halina uwezo kutunga Katiba kuyaondoa masuala yanayohusu Haki za Binadamu mpaka jopo la majaji 11 wa Mahakama ya Rufani kukaa na kubadilisha,na wakati huo huo masuala ya Haki za Binadamu si moja ya masuala ya Muungano,na katiba ya Zanzibar ndio muongozo mkuu wa Sheria nchi nzima lakini si sawa na ile ya Bara.

“Mnakumbuka kuna wakati Zanzibar ilitaka kutunga Sheria ya kuanzisha Mahakama ya Haki za Binadamu Zanzibar”,amehoji Jaji Makaramba kwa mawakili Zanzibar kuonesha ni namna gani suala la haki za binadamu lilivyo pasua kichwa kwa Zanzibar na Tanzania bara.

Kwa mujibu wa Sheria,matatizo baina ya serikali za Zanzibar na Tanzania yanahitaji kutatuliwa na Katiba Maalumu ya Muungano,ambayo ili ipatikane,inahitaji majaji wawili kutoka Tanzania Bara,na wawili kutoka Zanzibar na hii imepelekea kushindikana kupata fumbuzi nyingi za masuala mbalimbali yakiwemo ya Haki za binadamu toka sehemu hizi mbili za Muungano,lakini pia kesi ya sehemu hizi mbili haiwezi kupelekwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Onesmo Olengurumwa-Mratibu wa THRDC.

Mafunzo kwa Mawakili na Watetezi wa Haki za Binadamu,yatahitimishwa Ijumaa,Agosti 20 (Leo),baada ya kufunguliwa rasmi na jaji Mkuu wa Zanzibar,Omar Othman Alhamisi,Agosti 19.