March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAREKANI YAIPA TANZANIA MSAADA WA DOZI ZAIDI MILIONI MOJA ZA CORONA

Na Antony Benedicto

Dar es Salaam,Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umetangaza kuwa Marekani imetoa msaada wa zaidi ya dozi milioni moja za chanjo dhidi ya COVID-19 aina ya Johnson & Johnson, kama sehemu ya jitihada za kimataifa katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ameshudia hatua ya ya makabidhiano ya msaada huo kutoka kwa Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Balozi Wright.

“Marekani ina furaha kuchangia na Watu wa Tanzania zaidi ya dozi milioni moja za chanjo dhidi ya Covid-19. Marekani inasaidia kuiongoza dunia katika kulitokomeza janga hili, kujenga dunia iliyo salama zaidi na iliyokingwa zaidi dhidi ya kitisho cha maradhi ya kuambukiza.  Nchi zote, bila kujali hali zao za kiuchumi, zinahitaji chanjo zinazokidhi viwango vya juu” Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Donald Wright

Pia Marekani kupitia Ubalozi wao Nchini Tanzania  wamesema msaada huo ni kielelezo cha uimara wa ubia wa miaka 60 na dhamira ya dhati ya Marekani kwa Nchi ya Tanzania 

“Hiki ni kielelezo cha uimara wa ubia wetu wa miaka 60 na dhamira yetu ya dhati kwa Tanzania” Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Donald Wright

Katika makabidhiano hayo pia Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ambaye amekuwa akitoa maelekezo kwa wananchi kujitokeza kupata chanjo na kuwasihi wananchi kuchukua zaidi tahadhari kama wanavyoeleza wataalamu wa afya.