Polisi katika mji wa Utah wamekuta mtoto wa miaka 9 akiendesha gari huku mdogo wake mwenye umri wa miaka mine akiwa katika siti ya abiria na aliendesha gari hilo kwa umbali wa Kilometa 16 wakidai kuwa wanakwenda California kuogelea baharini.
Watoto hao waliondoka nyumbani saa tisa alfajiri wakati wazazi wao wakiwa bado wamelala na kuendesha gari katika barabara kuu mbili kabla ya kugongana na gari linguine na kisha kuvaana uso kwa uso na lori,hata hivyo watoto hao walikuwa wamefunga mikanda na hawakuumia.
Polisi walipata taarifa hizo baada ya dereva wa lori kuwapigia simu na kuwaeleza kuhusu tukio hilo.Wakati yote yakijiri wazazi wa watoto hao hawakufahamu lolote hadi walipoamshwa na polisi alfajiri hiyo na kupewa taarifa kuhusu ajali iliyotokea.
Hilo si tukio la kwanza kutokea katika mji wa Utah,mwaka jana mtoto wa miaka mitano alichukua na kuendesha gari la familia ili akanunue Lamborgini kwani baba yake amekataa kumnunulia
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS