Marekani imetangaza kumaliza mchakato wa kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi ulioanzishwa Desemba 14, 2020 ili kuiondolea vikwazo vya kiuchumi vilivyodumu kwa miaka 27.
Marekani imeeleza kuwa ofisi yake ya udhibiti wa mali za nje (OFAC) inafanyia marekebisho orodha hiyo ili kuondoa Sudan katika orodha ya kudhamini Ugaidi.
Sudan iliwekwa kwenye orodha ya Marekani baada ya shambulio la kwanza kwenye Kituo cha Biashara Ulimwenguni huko New York mwaka 1993, wakati Sudan ilipokuwa na vikundi kadhaa vya wapiganaji wa Kiislamu Pamoja na kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden.
Agosti 25, 2020 Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alifanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kuhusu tukio la kuorodheshwa kuwa mfadhili wa ugaidi.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS