March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAPENDEKEZO 65 YA UN YALIYOWEKWA KIPORO NA TANZANIA KUJADILIWA NA WANANCHI

SERIKALI ya Tanzania, imesema itayafikisha kwa wananchi mapendekezo 65 iliyokataa kuyapokea kutoka Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu uimarishwaji wa haki za binadamu, ili waamue hatima yake.

Akizungumza wakati anafungua kikao kazi cha kupitisha mpango mkakati wa Asasi za Kiraia, kuhusu utekelezaji wa mapendekezo 167 kati ya 252 ya UN, ambayo Serikali ilikubali kuyatekeleza, amesema wananchi ndiyo watakaoamua hatima ya mwisho juu ya mapendekezo hayo.

Amesema, Serikali ya Tanzania ilikataa kuyapokea mapendekezo hayo yaliyotolewa kwenye kwenye duru la tatu la Mchakato wa Tathimini ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UPR), kwa kuwa yalikuwa yanakinzana na mila na desturi za nchi.

“Baadhi ya mapendekezo haya 65 yalikuwa yanakinzana na katiba na mapendekezo mengine yalikuwa yanapingana na sera, sheria, mila na tamaduni za Watanzania au Afrika, katika haya mapendekezo hatujafunga mjadala tunaendelea kujadili ili Watanzania waseme kama mapendekezo hayo yanakinzana na katiba yetu tubadilishe au tuyaache,” amesema Dk. Ndumbaro na kuongeza:

Waziri huyo amesema “Watanzania wakishasema hayo sisi kwetu inabaki ni kutekeleza. Nasema hili kusisitiza kwamba sisi ni wawakilishi hivyo ni vizuri tutege masikio kwa wananchi wetu ambao tunawawakilisha tujue wanataka nini na hawataki nini.”