February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

TAKUKURU YAMUWEKA MANJI KIKAANGONI

Mfanyabiashara,Yusuf Manji

Mfanyabiashara maarufu Tanzania,Yusuf Manji anashikiliwa kwa mahojiano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU.Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru kamishna wa Polisi Salum Hamduni, amethibitisha kuwa wanamshikilia mfanyabiashara huyo kwa tuhuma tatu.


Manji alirejea nchini juzi jioni na alikamatwa na TAKUKURU baada ya kukamilisha taratibu za kuingia nchini.


Manji anakabiliwa na tuhuma za kukwepa kulipa kodi kati yam waka 2011-2015 kupitia Kampuni zake za Intertrade Commercial LTD Service na Golden Globe International Service Limited wakati wakifanya biashara na Shirika la umeme, kufanyika kwa udanganyifu wakati wa kununua kampuni ya Tigo na tuhuma nyengine inahusiana na mapato ya klabu ya mpira wa miguu ya Yanga kupitia kampuni yake ya Quality group wakati alipokuwa akiidhamini timu hiyo.


Yusuf Manji aliondoka nchini mnamo mwaka 2018 baada ya kuachiliwa huru na mahakama wakati alipokuwa akikabiliwa na tuhuma saba ikiwemo makosa ya uhujumu uchumi.