February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAMIA WAMUAGA PROF. NGOWI NA DEREVA WAKE

Mamia ya watu wameshiriki katika ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu chw Mzumbe, Prosper Honest Ngowi na wa dereva wake, Innocent Mringo, waliofariki dunia katika ajali ya gari maeneo ya Mlandizi, mkoani Pwani, tarehe 28 Machi 2022.

Ibada hiyo imefanyika leo Ijumaa, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Baba Paroko wa Kanisa la Romani Katholiki la St. Peter’s, Steohen Kaombe na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tabata Kuu, Kaanasia Msangi.

Mwakikishi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jerome Assey, amesema Taifa limempoteza bingwa katika masuala ya ushauri wa uchumi.

“Kwa kweli watu wengi ambao walikuwa wanamfahamu Prof. Ngowi na dereva wake wanasikitika sana, ni majonzi makubwa. Rais Samia anatoa pole nyingi kwa uongozi wa Chuo cha Mzumbe na familia zote mbili,” amesema Assey na kuongeza:

“Sote tunafahamu jinsi Prof. Ngowi alivyokuwa mbobezi katika suala la uchumi kwa kufanya kazi nzuri, bila shaka dereva wake Innocent amechangia. Kiukweli tumepoteza bingwa wa uchumi Tanzania,ni vigumu kuamini kwamba wote hawa wawili hatunao tena, itoshe kusema tuliwapenda sana lakini Mungu amewapenda zaidi, tuendelee kuwaombea.”

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, amesema, Prof. Ngowi alikuwa kiunganishi katika ya Chuo Kikuu cha Mzumbe na sekta binafsi kupitia kazi alizofanya za ushauri kuhusu masuala ya kiuchumi.

Mwakilishi wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Jonas Baraka, amesema wamepoteza mhadhiri mahiri aliyekuwa na mbinu bora za kuwafundisha na kuelewa masomo yake.

“Japokuwa alikuwa anafahamu lugha nyingi, alivyokuwa anafundisha alitumia misamiati ya kingereza ya kawaida ili wanafun,i waweze kuelewa somo na kulipenda. Alitambua ujuzi wa lugha ni mtu kufanya mawasiliano,” amesema Baraka na kuongeza:

“Alikuwa nguli na mwenye kipaji cha kuweza kukufungua machp na kuona kuona mema katika changamoto kali unazopotia za maisha. Pale unapolaumu atakufanya ubaini yale mema ambayo yapo katika changamoto unayopitia.”