February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAMBO YA KUZINGATIA KWA ASASI ZA KIRAIA WAKATI WA KUTAFUTA WAFADHILI

Mtaalamu kutoka Ubalozi wa Uswidi nchini Tanzania amezijengea uwezo Asasi za Kiraia visiwani Zanzibar juu ya masuala wanayopaswa kuyazingatia wakati wa kutafuta wafadhili wa kufadhili miradi ya mashirika hayo

Ametaja mambo ya msingi na yanayopaswa kuzingatiwa kwa upande wa Asasi za Kiraia ikwemo Asasi hizo kuwa na utayari pamoja na nyenzo.

Amesema katika kuandika nini taasisi yako inafanya iko wapi na malengo yake si lazima kuandika kurasa mia bali kurasa chache ambazo zinajitosheleza kwa mfadhili kuisoma nakuelewa taasisi yako inataka nini pia iwe na bajeti fupi kuwa fedha hiyo itafanya nini,pamoja na wasifu wa taasisi wa angalau kurasa moja ikieleza wewe ni nani,taasisi yako inafanya nini na inataka kufikia malengo gani.

Pia amezishauri Asasi za Kiraia kujaribu kuwaalika wafadhili katika shughuli zao muhimu hata kama hawawapi pesa,akitolewa Mfano kama taasisi haipati fedha kutoka ubalozi wa Uswidi unaweza kuwaalika.

Aidha amesisitiza ni lazima kuzingatia matakwa ya mfadhili anayewapa pesa akitoa mfano amefafanua kama mradi unafadhiliwa na Ubalozi wa Marekani ni lazima uandike barua pepe kwa Ubalozi wa Marekani kukuruhusu kuialika sweden katika shughuli yako,usifanye kwa kushtukiza.

Jambo lingine amesema ni lazima kwa mashirika kufahamu vipaumbele vya mfadhili ambaye unahitaji akupe fedha,akitolea mfano Uswidi amesema wana vipaumbele kadhaa ikiwemo haki za binadamu,usawa wa kijinsia,Elimu,Utawala Bora,uwajibikaji n.k,hivyo amesema ni muhimu kufahamu kabla hujamfuata mfadhili kuomba fedha.

Pia ameongeza kuwa lazima shirika au taasisi liwe ‘visible’ ,ameeleza unapokwenda kuomba ufadhili wa miradi mfadhili atataka kujua wapi ataiona au kuipata kwenye Televisheni,Radio au Mitandao ya kijamii.Amesisitiza kuwa ni wajibu wa taasisi kujifanya ionekane.

Akitolea mfano Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC ) kama mdau mkubwa wa Uswidi na huwa linapata fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambapo pia kuna ruzuku ndogo ndogo ambayo hutolewa kwa THRDC na hiyo ni kwa kukaa mezani na kushauriana kuhusu hizo fedha zinakwenda kufanya kazi gani na kusema kuwa hiyo ni fursa ambayo Azaki zinaweza kutumia kupata fedha kutoka kwa Taasisi ingine ambayo inapata fedha kutoka kwa wafadhili.