Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS wameiondoa Mali katika uanachama wa Jumuiya hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo juma lililopita ikiwa ni mapinduzi ya pili ndani ya mwaka mmoja.
Kiongozi wa mapinduzi ambaye amejitangaza kama Rais wa mpito,Kanali Assimi Goïta, alihudhuria mkutano uliofanyika mjinini Accra nchini Ghana.Waziri wa mambo ya nje wa Ghana,Shirley Ayorkor Botchwey amesema jumuiya hiyo imeitaka Mali kumteua Waziri Mkuu mpya ambaye anafaa kuwa rais mara moja ili kuheshimu kipindi cha mpito cha miezi 18 na uchaguzi ufanyike mwezi Februari.
Ghana ilisema utulivu wa Mali ni muhimu ili Afrika Magharibi ili iweze kudhibiti harakati za ugaidi katika kanda hiyo.Kanali Goïta alichukua mamlaka baada ya kuamuru kukamatwa kwa Rais Bah Ndaw na waziri mkuu Moctar Ouane.ambao waliwekwa kizuizini kwa siku kadhaa kabla ya kuamua kujiuzulu katika nyadhifa zao.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS