February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAKONDA AINGIA MITINI,KUBENEA AWEKA MKAKATI KUMPATA

Na: Anthony Rwekaza

Shauri namba 1/2022 lililopangwa kusikilizwa leo Februari 3, 2022 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni limeshindwa kusikilizwa kufuatia mjibu maombi namba tatu Paul Makonda kushindwa kufika.

Pia sababu nyingine ambayo imetajwa kuwa imepelekea kesi hiyo kushindwa kuendelea nj kutokana na ratiba ya kesi hiyo kuingiliana na shughuli nyingine za Mahakama.

Wakili Hekima Mwasipu ambaye alifika Mahakamani kumuwakilisha mleta maombi, akizungumza na Wanahabari kuhusu shauri hilo, amesema mjibu maombi wa tatu Paul Makonda hajafika Mahakamani hapo licha ya kufanya jitihada nyingi za kumfikishia taarifa ili aweze kuja Mahakamani.

Paul Makonda-Mtuhumiwa

Amesema mteja wake Saidi Kubenea ambaye ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Ubungo, aliwasilisha maombi Mahakamani ili kuruhusiwa kumshtaki Paul Makonda, akidai kuwa hatua hiyo imechukuliwa na mteja wake kufuatia mwendesha mashtaka wa Serikali (DPP) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kushindwa kutimza jukumu lao ipasavyo kwa kumfungulia mashtaka Poal Makonda.

Ameeleza kuwa kwahiyo maombi Kubenea ni kuwa anaiomba Mahakama kumruhusu kumshtaki Paul Makonda kupitia nafasi ya DPP kwa kuzingatia utaratbu wa kisheria unaotoa fursa hiyo, kwa kuwa Ofsi ya DPP ndiyo imepewa mamlaka ya kisheria ya kufungua mashauri ya Jinai isipokuwa zikifuatwa taratibu nyingine za kisheria.

Amesema kesi hiyo pia imeingiliana na ratiba nyingine za Mahakama, ambapo Hakimu Allon Lyamuya anayesikiliza shauri hilo alitakiwa kwenda kwenye majukumu mengine ya Mahakama, hivyo shauri hilo limeahirishwa mpaka Januari 8, 2022.

Saed Kubenea-Mwandishi wa Habari.

Aidha Wakili huyo amesema wanapanga kuiomba Mahakama kutoa wito mwingine ili waweze kufuata utaratibu wa kutumia magazeti kwa lengo la kueneza taarifa hizo ili ziweze kumfikia.

Shauri hilo limekuja kufuatia Mahakama Kuu, masijala kuu ya Dar es Salaam, kutoa ruhusa ya kufunguliwa kwa kesi ya jinai dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Ruhusa hiyo iliyotolewa Kwa njia ya maandishi iliripotiwa kutolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Joseph Luambano.

Awali Said Kubenea alifungua shauri namba 7/2021 akimshtaki Paul Makonda kwa matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo kuvamia kituo cha Runinga cha Clouds TV, wengine aliokuwa amewajumuhishi ni pamoja Mwendesha mashtaka na Mkurugenzi wa upelelezi wa Mkosa ya Jinai.

Lakini Desemaba 3, 2021 upande wa waleta maombi uliomba kuondolewa kwa shauri ilo Mahakamani kufuatia madai kuwa walikosea baadhi ya taratibu za kisheria katika kufungua shauri hilo, hivyo Mahakama ililiondoa shauri hilo.

Katika shauri hilo mjibu maombi namba tatu ambaye ni Paul Makonda ambaye amekuwa siku ameonekani kwenye vyombo vya habari, aliwai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, pia alikuwa miongoni mwa watia nia wa kiti cha Ubunge kwenye Jimbo la Kigamboni Jijini Dar es salaam kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), lakini pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.