Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ametoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na uhalifu katika jiji hilo kuacha mara moja na wasalimishe silaha katika vituo vya polisi.
Kauli ya Makalla inakuja siku chache baada ya matukio mawili ya kutumia silaha kutokea jijini humo ambapo katika tukio la awali watu waliojihami kwa silaha za moto walimvamia mtu mmoja katika eneo la Mbezi na kumua kwa risasi kabla ya kupora fedha alizokuwanazo,huku tukio la pili lilikihusisha mfanyabiashara mmoja wa eneo la Mabibo aliyevamiwa eneo lake la biashara na kupigwa risasi ambapo wahalifu hawakufanikiwa kupora fedha.
“Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa kama ambavyo alisema rais wasijaribu,tunawaonya majambazi wote na wahalifu wote katika mkoa huu kwa hiari zao waache mara moja”,ameeleza RC Makalla mbele yay a wandishi wa habari.
Makalla aliyeteuliwa kuongoza mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni na rais Samia Suluhi amekaribishwa Dar es Salaam kwa matukio hayo ya uhalifu huku pia Kamanda wa Polisi Kanda wa kanda hiyo akiwa mgeni jijini humo.
Rais Tanzania Samia Suluhu amenukuliwa mara tatu katika matukio tofauti akigiza polisi kukomesha matukio haya yanayoibua taharuki na kutia doa jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
“Miuongoni mwa sifa tutakazotumia kuteua na kutengua uteuzi ni paja kushindwa kukomesha uhalifu” alisema Rais Samia alipowaapisha wakuu wapya wa mikoa juma lililopita.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA